Apple wametambulisha roboti yao waliyoipa jina la Daisy. Roboti huyo anauweza wa kufumua simu 200 ndani ya muda wa saa moja.
Roboti huyu anasaidia mpango mzima wa Apple wa kusaidia mazingira, kwani baadhi ya vipuli vinavyokuwa kwenye simu vinaweza kutumika tena (recycled).
Ndani ya simu janja za kisasa kuna vitu mbalimbali vyenye thamani kubwa, hii ni pamoja na vipuli vilivyotengenezwa kwa kutumia madini kama vile dhahabu, shaba, platinum, lithium, na mengine mengi. Vipuli hivyo vinaweza kuyeyushwa na kwa kutumia madini hayo kutengeneza tena upya vipuli vingine.
Roboti Daisy ataweza kutambua aina ya iPhone na kisha kupitia data alizowekewa kuweza kufahamu jinsi vipuli vimepangwa ndani ya simu hiyo na hivyo kuweza kuvifungua vyote kwa usahihi.
‘Kwa kila simu 100,000 za iPhone roboti Daisy ataweza kupata kilo 1,900 za alumini, kilo 710 za shaba.’