Daktari mpasuaji akiri kuweka nembo katika maini ya wagonjwa wake

0
Sambaza

Daktari Simon Bramhall mtaalamu wa upasuaji nchini Uingereza amekiri kufanya makosa ya kuweka nembo yake katika maini ya wagonjwa wake aliowafanyia upasuaji.

Daktari huyo mwenye umri wa miaka 53 amekiri kuwa ameacha herufi A na B katika maini ya wagonjwa wake baada ya kuwafanyia upasuaji.

nembo katika maini

Huyu ndio Dk Saimon: Daktari mpasuaji akiri kuweka nembo katika maini ya wagonjwa wake

Daktari Simon alifanya makosa hayo katika Hospitali ya Queen Elizabeth huko Brmingham mwezi Februari na Agosti mwaka 2013.

SOMA PIA:  Google na Microsoft waungana katika vita dhidi ya mitandao ya mafaili ya wizi

Daktari huyo amekiri mbele ya mahakama kuwa aliandika herufi A na B kwa kutumia mionzi katika maini ya wagongwa wawili aliowafanyia upasuaji mwaka 2013 bila ya ridhaa yao.

Daktari huyo ameachiwa huru kwa dhamana hadi kesi yake itakaposikilizwa tena Januari mwaka 2018.

Nembo hizo iligunduliwa katika zoezi la uchunguzi kwa mgonjwa mmoja ambae alifanyiwa upasuaji na daktari Simon.

Facebook Comments
Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com