Datally, app kutoka Google: Njia ya kuokoa utumiaji data wa apps kwenye simu yako

0
Sambaza

Fahamu app mpya kutoka Google, imepewa jina la Datally na inalenga kuwa njia ya kuokoa utumiaji data wa apps mbalimbali kwenye simu yako.

Muonekano wa app ya Datally Njia ya kuokoa utumiaji data wa apps kwenye simu yako

Muonekano wa app ya Datally: Njia ya kuokoa utumiaji data wa apps kwenye simu yako

App hii itakuonesha utumiaji wa data (intaneti) unaofanywa na apps mbalimbali na pia kukupa uwezo wa wewe kuzidi kuzibana na kusitisha utumiaji huo kwa apps hizo.

Kingine ndani ya app hiyo ni pamoja na uwezo wa kuona huduma za intaneti ya WiFI zilizokaribu (kama umewasha eneo la WiFi kwenye simu yako) na kukuonesha huduma zenye kasi nzuri zaidi.

SOMA PIA:  Google yawa kampuni ya kwanza ya kigeni ya Intaneti kuzindua huduma zake Cuba

Na watumiaji wa app hiyo wengine kama wameacha ‘comment’ kuhusu huduma za WiFi unazoziona kwenye app hii basi utaweza kuziona pia – mfano wengine wanaweza wakawa wameponda huduma ya WiFi flani n.k.

App hii inapatikana duniani kote mara moja. Huu ni muendelezo wa hatua zinazochukuliwa na Google kuhakikisha vitu ambavyo tayari vinawezekana kwenye Android vinaweza fanyika kwa urahisi zaidi.

Ata kama app inatumia data muda ambao wewe hautumii simu au app hiyo husika, app hii itakupa repoti kuhusu utumiaji huo.

SOMA PIA:  Apple Kuongeza Dau Kwa Google Ili Kubakia Kuwa Sehemu Kuu Ya Matafuto (Default Search Engine) Katika iOS!

Wengine wanaweza kusema tayari kuna eneo la kwenye mipangilio (settings) ya Android ambapo unaweza kuona hili. Hii ni kweli, ila si watu wote huwa wanaona ni njia rahisi kwenda kule.

Kupitia app hii Google wanaamini itakuwa rahisi zaidi kwa mtumiaji yeyote wa simu za Android kuweza kufahamu na kusimamia utumiaji wa data unaofanywa na apps za kwenye simu yake.

| Download Datally – Google PlayStore |

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com