Shirika la Maji safi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco) limezindua mita mpya za maji ambazo malipo yake yatafanyika kabla ya matumizi (prepaid meters).
Mita hizo zinafanya kazi kama ilivyo kwenye mita za LUKU ambapo mtumiaji atatakiwa kulipia kiasi anachotaka. Baada ya kufunga mita hizo, Dawasco watakuwa wanazifuatilia kupitia mfumo maalum wakiwa ofisini kwao hivyo hakutakuwa na ufuatiliaji wa wateja nyumbani.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhe. Prof. Makame Mbarawa amesema mita hizo za malipo ya kabla zitasaidia kuleta nidhamu katika matumizi ya maji na kuliongezea shirika mapato.