Diski ya 8TB Kutoka Seagate Yaingia Sokoni!

0
Sambaza

seagate-logoMwezi wa tisa tuliandika kuhusu ujio wa diski ya 8TB kutoka Seagate na wiki hii diski hiyo imeingia sokoni rasmi kwa ajili ya watumiaji wa kawaida kama mimi na wewe.

Diski hii ya 8TB kutoka kwa Seagate ilisubiliwa kwa hamu kutokana na ubora wake pamoja na bei rahisi iliyotegemewa kuja nayo kulinganisha na diski za ukubwa huo kutoka kwa kampuni zingine.

8TB hiyo imeingia dukani kwa takribani dola za Marekani 270, ambazo ni takribani Tsh laki 4.7, hii ni rahisi kwani hadi miezi michache iliyopita diski za ukubwa wa TB 6 zilikuwa zinauzwa kwa si chini ya laki 5 wakati za TB 4 zilikuwa zinauzwa kwenye laki 3 na ushee.

SOMA PIA:  Ripoti: Biashara ya mtandaoni yaongezeka kwa wananchi wa Kenya

Hivyo ujio huu wa diski hizi utasababisha kushuka kwa bei ya diski zingine zote. Unaweza kusoma zaidi kuhusu diski hii kwenye habari yetu ya mwezi wa tisa -Bofya http://teknokona.com/2014/09/01/seagate-waanza-kuuza-diski-ya-tb-8/

Je unaweza fikiria kutumia diski moja yenye ukubwa wa TB 8?

Yaani kama unafilamu zenye ukubwa wa 800MB kila moja inamaanisha kuijaza utaitaji zaidi ya mafaili 1,250,000 kujaza diski hii moja. Ila kwa watumiaji kompyuta zao kwa ajili ya kucheza magemu makubwa basi diski ya TB 8 itakuwa inaitajika kwa sana tuu, kwani magemu mengi huchukua nafasi kubwa sana. Ila ata kwa matumizi hayo pia, kujaza diski ya TB 8 ni ishuuuuuu!

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com