Dokta Aliyepona Maambukizi Ya Ebola Aikosoa Mitandao Na Wanasiasa!

0
Sambaza

ebola-doctor-craig-spencer

Dkt. Craig Spencer ambaye alipata maambukizi ya Ebola na kupona ugonjwa huo, anasema wanasiasa na mtandao kwa ujumla ulikuza sana jambo hilo liliomtokea.

Janga la ebola lilizuka februari 2014 katika baadhi za nchi za magharibi mwa afrika. Licha ya hivyo ugonjwa huu hatati ulifika hadi marekani  kwa sababu madokta na ma nesi wengi wa marekani walipata maambukizi ya ugonjwa huu wakati wakijaribu kuokoa wale watu wenye maambukizi.

Dkt. Craig Spencer amabaye alikua anafanya kazi na madaktari wenzie nchini Guinea, alipata maambukizi ya huo ugonjwa na kurudi nao nchini marekani bila yeye kujua. Dokta huyu alikua hapendi kutoka nje na mara nyingi alikua akiendesha gari lake kutumia njia za chini na hii ni kabla ya dalili za ugonjwa hazijaanza kujionyesha

26SPENCER-Y-articleLarge

Dkt. Spenser Akiruhusiwa kutoka hospitali baada ya kupona

Dkt. Spenser ameweka wazi kuwa matembezi yake katika mazingira ya kijamii yalikosolewa kabla ya kuwa na uhakika kama ana ebola. Anasema wanasiasa na mitandao ndio iliomkosoa sana sana wakidai kuwa anaweka maisha ya watu wa New York (NY) hatarini. Napia baadhi ya watu walimuita mdanganyifu na wengine wakimuita shujaa.

”Baada ya utambuzi wa ugonjwa wangu, Mitandao na wanasiasa wangetumia mda huo kuwa elimisha wanajamii juu ya janga la ebola lakini wao walitumia mda huo kuangalia maisha yangu kwa ujumla na wapi naenda au nini nafanya” – alisema dokta Spenser

Dokta huyo amedai kuwa alijibu mahitaji yake kwa watu wa Guinea na kwenda kuwapa msaada walio uhitaji na pia anajiona mwenye bahati ya ajabu baada ya kupona maambukizi ya ugonjwa huo tishio. Dokta alisema mitandao ulikuza mambo alipopata ebola na ukazima habari zote baada ya yeye kutoka hospitali.

SOMA PIA:  Flippy: Roboti mahususi kwa ajili ya upishi wa 'Burger'! #Teknolojia

Alisema hata wanasiasa walichukulia jambo hilo kwa manufaa na hata hawakutoa sapoti yoyote kwake. Anamkosoa Gavana Andrew M. Cuomo wa New York na Gavana Chris Christie wa New Jersey kwa majibu/uitikio wa ugonjwa wake.

Ugonjwa huu wa ebola bado ni tishio Afrika na umeambukiza maelfu ya watu mpaka sasa  pia umesababisha vifo vya zaidi ya watu 14,000. Wanasayansi wanazidi kujikita katika kutafuta chanjo na dawa rasmi yenye nguvu.  Swali la msingi, kwenye ulimwengu huu wa teknolojia za habari za haraka hii ikiwa na pamoja Twitter na Facebook, je mtu anaweza kuwa na maisha binafsi (Privacy)?

Ningependa kusikia kutoka kwako pia tafadhali ungana nasi kupitia kurasa zetu za Twitter, Facebook Na Instagram

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com