Namna gani unaweza kupakua video/picha kwenye Instagram

1
Sambaza

Wengi wetu tunatumia Instagram kwa maelengo mbalimbali kama kibiashara, kujua yanayoendelea kutoka kwa watu mbalimbali, n.k ila uwezo wa kupakua kile ambacho umekiweka tumegundua si wengi wanafahamu au hata kama inawezekana.

Tunajua njia zipo nyingi ila leo fahamu moja ya njia za ku download video za Instagram

Kile ambacho unakiweka kwenye instagram iwe picha/video inawezekana kabisa kukipakua na ukawanacho kwenye simu yako kama ulikiondoa kwa bahati mbaya kwenye simu yako. Ni muhimu kuhakikisha kuwa simu yako ina nafasi ili kuweza kupakuwa kitu unachotaka kutoka Instagram.

SOMA PIA:  MASTODON:Ufahamu mtandao mbadala wa Twitter unaokuja kwa kasi

Jinsi ya kupakua picha au picha jongefu kutoka Instagram

 • Pakua programu wezeshaji ijulikanayo kama RapidSave; ni bure (haiuzwi).

  Muonekano wa app ya RapidSave

 • Fungua Instagram kisha nenda kwenye picha/video unayotaka kuipakua. Nakili link ya picha au video ambayo unataka uiapkue kutoka Instagram.
  download video za instagram

  Namna ya kunakili link ya picha au video

 • Fungua app ya RapidSave kisha paste ile link uliyocopy kutoka Instagram. Baada ya kupaste link bofya Preview halafu bonyeza Save.

  Kama ukosea kupaste link bofya close na kisha rudi Instgram na kisha unakili upya link ya picha/video unayotaka kuishusha.

 • Ingia kwenye Gallery kuweza kuona picha/video uliyoipakuwa kutoka Instagram.

Kwa uwezo wa teknolojia karibu kila kitu kinawezekana na endelea kutumia Instagram katika manufaa yako na wale wanakufuatilia kwenye Instagram. Je, kuna njia gani zingine huwa unazitumia?

Play Store: RapidSave|App Store: RapidSave

Vyanzo: iDownloadBlog, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com