Dropbox wadukuliwa; Mamilioni ya akaunti hatarini

0
Sambaza

Imegundulika kwamba zipo taarifa za akaunti zaidi ya milioni 68 ambazo ziliibiwa katika tukio la udukuzi dhidi ya mtandao wa Dropbox miaka kadhaa iliyopita.

Taarifa hizi zinajumuisha barua pepe na nywila za watumiaji wa mtandao huo ambao unajihusisha na uhifadhi katika mtandao.

Dropbox wadukuliwa

Inasemekana kwamba taarifa hizi ziliibiwa mwaka 2012 ambapo wadukuzi walitumia taarifa za wafanyakazi zilizoibiwa kujipatia nyaraka ambazo zilikuwa na taarifa hizi, ingawa Dropbox hawakuutarifu umma juu ya tukio hili mwanzoni lakini pia hata walipotoa taarifa walisema ni barua pepe tu ambazo zilikuwa zimeibiwa kinyume na ukweli halisi.

SOMA PIA:  Drone ya kubebea mzigo wa zaidi ya kilo 200 yaundwa

Dropbox sio mtandao wa kwanza kufanyiwa udukuzi wa namna hii!?

Tayari yapo makampuni makubwa kadhaa ambayo pia yalidukuliwa na taarifa za wateja zikaanikwa katika mnada wa mtandaoni, Myspace na LinkedIn ni moja ya makampuni ambayo tayari yalishawahi kushambuliwa na taarifa za wateja wao ambazo zilibiwa kuwekwa mtandaon baada ya muda.

Je wewe pia utakuwa ni muhanga wa janga hili? na kama ndiyo ni hatua gani uchukue??

Kama ulijiunga na Dropbox mwazoni wa mwaka 2012 au kurudi nyuma basi bila shaka unatakiwa kubadili nywila yako katika mtandao huu, hata hivyo mtandao huu umechukua hatua kwaajiri ya kuwatahadharisha watumiaji ambao nywila zao zipo kati ya zile zilizoibiwa.

SOMA PIA:  Polisi nchini Dubai yafanyia majaribio mbinu mpya ya kuimarisha usalama

Kufahamu kuhusu DropBox na Jinsi ya kutumia -> DropBox ni nini?

Teknokona inaendelea kukusihi kuhakikisha kwamba hautumii nywila moja katika mtandao zaidi ya mmoja pia inapowezekana basi hakikisha unatumia two factor authentication method  hii itasaidia katika majaribio ya udukuzi.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com