DTEK50: BlackBerry waja na Simu iliyo juu zaidi Kiusalama Duniani

0
Sambaza

Kila unapofikiria mwisho wa simu za BlackBerry umefikia ndio BlackBerry wanakuja na kitu kipya cha kukuonesha bado wapo katika biashara ya simu.

Fahamu kuhusu simu yao mpya, DTEK50, simu inayosemekana inafaa kupewa sifa ya kuwa simu salama zaidi dhidi ya udukuzi n.k.

DTEK50

Muonekano wa simu ya BlackBerry DTEK50

Simu hii mpya kutoka BlackBerry inayofahamika kwa jina la DTEK50 itaingia rasmi sokoni mwezi wa nane mwaka huu na kwa kiwango cha bei cha takribani dola za kimarekani 300 (takribani Tsh Tsh 657,000/= | Ksh 30,400/=)

SOMA PIA:  Jinsi ya kusambaza kitu chenye ujazo mkubwa kwenye WhatsApp #Maujanja

Nini kipya?

Hii ndio simu ya kwanza ya Android iliyo ya kugusa tuu(touchscreen) kutoka BlackBerry. BlackBerry ndio wanasifika zaidi duniani kwa kuwa na mifumo ya kiteknolojia salama zaidi ya kiusalama wa data dhidi ya udukuzi katika simu.

Na katika BlackBerry DTEK50 inaonekana wanaona kutumia Android ambayo tayari ni programu endeshaji maarufu zaidi ukichanganya na teknolojia za BlackBerry za usalama basi simu hii inaweza jipatia umaarufu kwa watu na mashirika yanayojali usalama wa data zao zaidi.

blackberry dtek50 neon

Simu hii ndiyo ilikuwa mwanzo inafahamika kwa jina la siri la BlackBerry Neon

Sifa za kiundani

  • Kioo cha inchi 5.2 cha uwezo wa HD wa 1080p
  • Prosesa ya Snapdragon 617
  • Kiasi cha RAM cha GB 3
  • Diski Uhifadhi (storage) GB 16 huku ukiwa na uwezo wa kutumia memori kadi
  • Betri lisilo la kutolewa la mAh 2,610
  • Kamera ya selfi ya MP 8 huku ile kuu ikiwa ya MP 13.
SOMA PIA:  WhatsApp haina chanzo cha kuingiza Pesa mpaka sasa #Uchambuzi

Je itafanikiwa?

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya BlackBerry ameshashusha kiasi cha mauzo ya simu kwa mwaka ili biashara ya simu ionekane inaleta maana kwao. Mwanzoni wakati wanatambulisha simu janja ya BlackBerry Priv alisema ili wao waweze kuendelea na biashara ya utengenezaji simu basi ni lazima mauzo ya simu zao yawe si chini ya simu milioni 5 kwa mwaka…lakini sasa amebadilika na kusema mauzo yawe si chini ya simu milioni 3 kwa mwaka.

SOMA PIA:  Picha za Samsung Galaxy S9 na S9 Plus Zavuja

Kwa simu hii ambayo ata kibei ni nafuu kidogo ukilinganisha na zilizotangulia na hasa hasa ikionekana inavutia zaidi ata mashirika nyeti mpango huo wa kimauzo unaweza kufikiwa.

Soma Pia – BlackBerry kuja tena na simu 3 zinazotumia Android

Je unaionaje simu hii? Inavutia? Je unadhani itafanikiwa kimauzo?

Vyanzo: Mitandao mbalimbali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com