Dubai ni mji wa kwanza Duniani kuwa na Fonti zake kwenye Microsoft Office

0
Sambaza

Kupitia Dubai Font, Dubai umekuwa mji wa kwanza duniani kuwa na aina ya herufi za chapa yake yenyewe (Font), serikali ya nchi ya Umoja wa Falme za kiarabu (United Arab Emirates UAE) ilitangaza Jumapili iliyopita.

Fonti hiyo itajulikana kwa jina la ‘Dubai Font’ na itakuja kwa herufi za kiarabu na kilatini na itakuwa katika lugha 23 tofauti duniani.

Hatua hii imekuja kwa kushirikiana na kampuni ya Microsoft na kwa sasa itapatikana kwa watumiaji wapatao milioni 100 wa Microsoft Office 365 duniani kote.

SOMA PIA:  Instagram Yaja Na 'Sticker' Kama Snapchat!

dubai font

Crown Prince Hamdan bin Mohammed al-Maktoum alieleza hatua hiyo ni mradi wa kipekee utakaosaidia kuonyesha urithi na utamaduni nchi ya Umoja wa Falme za kiarabu (UAE).

Dubai imekuwa mstari wa mbele katika kujitangaza kwa namna nyingi kwa nchi mbalimbali duniani kuhusu vivutio vilivyo katika nchi yao ya Umoja wa Falme za kiarabu (UAE). Mwaka 2016, watalii milioni 14.9 walitembelea mji wa Dubai.

Nini maoni yako kuhusiana na taarifa hiyo. Je nawe ungependa nasi tuwe na Fonti yetu katika Microsoft office? Kama ndio jina gani ungependa litumike, Twiga font, Kilimanjaro font, Serengeti Font au…Tupe maoni yako na jina ulipendalo.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com