DuoSkin: Microsoft na MIT waja na tatoo inayoweza kuendesha Simu au Kompyuta

0
Sambaza

Kuwa na tatuu (tatoo) mkononi inayoweza ku’control simu au kompyuta? Jambo liko kama kimuvi zaidi lakini tayari Microsoft na chuo cha MIT wanakuja na teknolojia hiyo. Fahamu kuhusu DuoSkin.

duoskin MIT Microsoft

Muonekano wa tatuu hiyo ya DuoSkin

Watafiti wafanikiwa kutengeneza tatoo ya madini ya chuma (metallic) yenye uwezo wa kuendesha (control) simu, kompyuta au kifaa kingine chochote kilichounganishwa na tatuu (tatoo) hiyo.

Wanafunzi wa PhD wa chuo cha MIT (Michigan Institute of Technology) wakishirikiana kitengo cha utafiti cha Microsoft wamefanikiwa kutengeneza tatuu ya kwanza iliyotumia madini ya chuma.

Tatuu hiyo kwa sasa ni ya muda mfupi tuu, yaani ‘temporary’….

Utakapoivaa inageuza eneo la mkono wako kuwa kama eneo la kipanya cha mguso kwenye ‘laptop’. Na eneo hilo linalofunikwa na tatuu hiyo litaweza badilika rangi kulingana na joto la mwili wako.

Teknolojia kuu zilizotumika katika utengenezaji wa tatuu hizo ni pamoja na chip za NFC na LED.

Kwa sasa inategemewa teknolojia hiyo itafanyiwa maboresho na tunaamini miaka si mingi tunaweza jikuta tunanunua tatuu hizi. Vipi mtazamo wako?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Mmoja wa waanzilishi wa Android kuja na simu ya kushindana na iPhone
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com