Elari NanoPhone C: Hii ndio simu ndogo zaidi duniani

0
Sambaza

Simu yenye umbo ndogo zaidi duniani yazinduliwa nchini India, inafahamika kwa jina la Elari NanoPhone C.

Simu ya Elari NanoPhone si simu janja bali ni simu ya kawaida na imetambulishwa rasmi nchini India.

Simu hii ndio inachukua sifa ya kuwa simu yenye umbo dogo zaidi duniani na tayari watumiaji simu nchini India wanaweza kuinunua simu hiyo.

Elari NanoPhone C simu ndogo duniani

Inauzwa kwa takribani Tsh 137,000/=

Sifa zake kuu,

  • Ni simu ya kawaida, si simu janja na hivyo kazi zake kuu ni kwa matumizi ya kawaida. Hakuna whatsapp wala facebook ndani yake.
  • Inaukubwa wa inchi 1.4 kwa upana, inchi 3.71 kwa urefu, na inchi 0.2 kwenye unene. Ina uzito mdogo wa gramu 30 tuu.
  • Inakuja na uwezo wa kukubali memori kadi ya hadi ukubwa wa GB 32, inakuja na uwezo wa kucheza mafaili ya mfumo wa MP3 hivyo nafasi hiyo inafaa kwa ajili ya muziki.
  • Pia inakuja na uwezo wa redio za mfumo wa FM, pia uwezo wa kurekodi sauti hii ikiwa ni pamoja na kurekodi maongezi ya simu.
  • Ina uwezo wa kuhifadhi namba za simu 1000, pia betri lake linaweza dumu na chaji kwa muda wa siku nne.
Elari NanoPhone C

Elari NanoPhone C: Simu hii itakuja kwenye rangi tatu.

Uwezo wa Bluetooth pia upo ndani yake, nje ya hapo hakuna kingine kikubwa sana kuhusu simu hii. Simu hii inalenga kuwa simu muhimu kwa watu wasio na uhitaji wa simu yenye mambo mengi sana, lakini pia inaweza ikawa simu nzuri kuwa nayo sambamba na simu janja nyinginee unayotumia.

SOMA PIA:  'Wasiojulikana' waiba simu za iPhone X zenye thamani ya 826 milioni

Je una mtazamo gani juu ya simu hii? Bado taarifa za upatikanaji wake nje ya india hazijatoka ila kama ikifanikiwa zaidi kimauzo nchini humo itakuwa rahisi simu hizo kusambaa zaidi.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com