Elon Musk: Nenda kokote duniani ndani ya lisaa, safiri kwenda Mirihi(Mars)

Elon Musk: Nenda kokote duniani ndani ya lisaa, usafiri kwenda Mirihi (Mars) unakuja

0
Sambaza

Nenda kokote duniani ndani ya lisaa? Muanzilishi wa kampuni mashuhuri katika utengenezaji wa magari yanayotumia umeme Bwana Elon Musk atangaza utengenezaji wa roketi ya kisasa zaidi kwa ajili ya safari za anga.

Kampuni ya SpaceX ipo katika utengenezaji wa rokoti mpya zenye lengo la kufanikisha safari za anga za juu na hadi kuwafikisha binadamu katika sayari zingine kama vile Mars.

watch Bwana Elon Musk amesema anataka kufikia 2022 safari ya kwanza ya mizigo kwenda sayari ya Mirihi (Mars) mwaka 2022. Baada ya hapo kutakuwa na safari nyingine mwaka 2024 itakayoweza kubeba wanadamu. Hii juu ni post yake ya Instagram inayoonesha mfano wa muonekano wa sayari ya Dunia kutoka kijiji kitakachokuwepo kwenye sayari ya Mirihi.

INAYOHUSIANA  Ijue ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner

Bwana Musk alikuwa anazungumza nchini Australia na aliwaonesha watu mpango mzima wa kufanikisha zoezi la kuanzisha makazi katika sayari ya Mirihi.

ellon musk makazi mars Nenda kokote duniani ndani ya lisaa

Elon Musk akionesha picha ya mfano wa makazi (koloni) la kwenye sayari ya Mars

SPACEX BFR Usafiri wa anga

Muonekano wa kimchoro wa sehemu kuu za usafiri wa BFR

Roketi mpya ambayo ipo katika matengenezo iliyopewa jina la BFR (Big Flying Rocket) inajengwa kufanikisha;

  • Safari za ndani ya dunia kutoka mji mmoja katika nchi moja kwenda mji mwingine katika nchi yeyote duniani kote itachukua ndani ya dakika 30.
  • Kusafirisha mizigo kwenda kituo cha kimataifa cha anga (hiki kipo anga ya juu kabisa – International Space Station)
  • Kuwezesha safari za watu na mizigo kwenda sayari ya Mirihi

http://straightarrowhomeinspection.com/contact_us.html Kwa sasa tupo kwenye utengenezaji wa vipuli vya BFR, kuanzia mwakani tunategemea kuanza uundaji mzima. – Elon Mask

where can i buy disulfiram in the uk Pia Musk ametangaza kuhusu biashara ya utalii kufika hadi kwenye anga ya mwezi na kurudishwa duniani. Hadi sasa tayari watu wawili ambao hawajawataja majina wameshalipia kiasi cha fedha na wanapitia maandalizi ya safari hiyo. Safari inategemewa  kufanyika ndani ya miaka michache ijayo.

Kuhusu lengo lake la kutengeneza makazi katika sayari ya Mirihi amesema rokoti hii inategemea kuwezesha usafirishaji wa watu kwa bei nafuu kwa kuwa inakuwa muendelezo wa teknolojia ya roketi zinazorudiwa kutumika. Lengo ni kusafirisha mamia ya watu kwa mfululizo wa miaka 40 hadi 100 ili kufanikisha idadi ya watu milioni 1 kuishi katika sayari hiyo.

INAYOHUSIANA  Rais Kagame azindua gari la kwanza lililounganishwa Rwanda

Lengo ni kwamba watakaopelekwa kwenye awamu ya kwanza kwenda kwenye sayari ya Mirihi watakuwa pia wanasayansi watakaoweza kutengeneza teknolojia ya kusaidia kutengeneza mafuta kwa ajili ya kuwezesha rokoti hiyo kufanya safari ya kurudi duniani.

Kingine kikuu kuhusu roketi ya BFR ni kwamba ina uwezo wa kujazwa mafuta zaidi ikiwa angani.

Vipi je wewe umelichukuliaje wazo la Bwana Ellon Musk?

Vyanzo mbalimbali: TheGuardian,  The Verge na vingine mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.