Emoji mpya 2017 zinakujia, zifahamu mpya zinazokuja

0
Sambaza

Kuna kautamaduni wa takribana kila mwaka wa tume inayosimamia ubunifu na utumiaji wa Emoji ndani ya shirika la Unicode kutambulisha emoji mpya. Kwa mwaka huu kuna mpya kadhaa.

Unicode ni shirika linalosimamia utumiaji wa teknolojia za alama mbalimbali kwenye simu na jinsi gani utumiaji wa alama hizo unafanikisha nini.

Kutakuwa na Emoji mpya 56 mpya (angawa kiujumla kutakuwa na emoji 69 – ukijumlisha na za utofauti wa jinsia).

Kikubwa zaidi ni kwamba kutakuwa na Emoji ya panzi – tena panzi aliyepata umaarufu sasa hivi kwenye mitandao ya kijamii kutokana na miguu yake….watu wakisema ni mizuri sana.

SOMA PIA:  Maboresho: Instagram Direct yazidi kunogeshwa .

emoji wa panzi

Kuna Emoji mbalimbali zilizotengenezwa zilizotengenezwa kuwakilisha wahusika mbalimbali maarufu wa filamu na stori za zamani. Hii ni pamoja na filamu maarufu ya Hulk, filamu za Aladini, Dracula, na zimwi la bahari (Mermaid).

emoji mpya

Na pia kuna Emoji nyingi zaidi zimeongezwa za sura za tabasamu na uchokoziiii..

emoji mpya 2017

Baadhi ya Emoji mpya 2017

Katika kipindi chochote kuanzia sasa tegemea apps mbalimbali na simu kuja na masasisho (updates) yanayojumuisha Emoji hizi mpya.

Tazama video hii fupi kuzijua Emoji mpya nyingine zaidi zilizopitishwa kutumika.

SOMA PIA:  Google kufanya masasisho ya kwenye apps zake kuongeza usalama

Vipi, je katika Emoji hizi ulizoziona ni zipi zimekuvutia zaidi?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com