iOS: Mabadiliko Emoji ya Kusali na Emoji kwa Wapenzi wa Jinsia Moja

iOS: Mabadiliko kwa Emoji ya Kusali na Kuletwa Kwa Emoji za Wapenzi wa Jinsia Moja

0
Sambaza

Masaa machache baada ya Apple kuleta emoji mpya katika toleo la iOS 8.03 watu waanza kulalamika kwenye mitandaoni.  Emoji mpya zilizoletwa kwa watumiaji wa iPhone, iPad na iPod touch zilizopokea toleo hilo la iOS zimekuja na mambo mengi mapya hasa hasa ikiwa ni muongezeko wa rangi mbalimbali za emoji hizo kulingana na aina za watu.

Hii inamaanisha kuna Emoji zenye rangi za kiafrika, wazungu, na ata watu kutoka bara la Asia yaani China na zinginezo.

Ila baada ya kuanza kutumia watu wamegundua kuna mabadiliko mengine yamefanyika yasiyokuwa na ulazima kama vile kuondoa alama za mwanga kama ‘upako’ vile kwenye emoji ya kusali. Na watu wamekasirishwa na uamuzi huo wakidai kwa nini wafanye mabadiliko yasiyokuwa na ulazima…. na pia kuna ata wengine wakaanzisha mazungumzo ya kudai emoji hiyo haikuwa ya kusali bali ni watu wawili wakisalimiana kwa mikono, yaani maarufu kwa jina la kupeana ‘High Five’  🙂

INAYOHUSIANA  VIdeo za makundi kwenye Instagram sasa ni rasmi

Tazama mabadiliko hayo hapa;

'Upako' au alama za mwanga...umeondolewa kwenye toleo jipya la Emoji

http://forensor-project.eu/author/zeesmi/ Kushoto ni muonekano wa zamani na kulio ni muonekano mpya wa Emoji hiyo. ‘Upako’ au alama za mwanga…umeondolewa kwenye toleo jipya la Emoji

Emoji kwa ajili ya mashoga?

Ndiyo, Apple wanaodai mara zote ya kwamba wanaunga mkono haki za mashoga – wapenzi wa jinsia moja, na hii ikiwa ni pamoja na bosi wao Bwana Tim Cook kukiri tayari ya kwamba yeye anashiriki mapenzi ya jinsia moja ( Soma -> Tim Cook wa Apple asema “Najivunia Kuwa Shoga”) , sasa wameleta emoji kwa ajili ya kuonesha hali hiyo. Baadhi ya emoji za kifamilia zipo zitakazokuwa zinaonesha familia zenye wazazi wa jinsia moja pamoja na watoto. Pia kutakuwa na watu wa jinsia moja walioshikana mikoni kwa pamoja, zamani zilikuwa zipo za hivyo za jinsia tofauti tuu.Emoji_apple_ushoga_tanzania

http://dianaarand.com/?work=the-kiss-remix Soma Pia;

Tom Cook Atangaza na Kukubali rasmi ya kuwa yeye ni shoga

Apple waleta iOS 8.3 Iliyojaa Emoji Mpya

http://reginafasteners.com/wp-json/oembed/1.0/embed?url=http://reginafasteners.com/affliates/ Je una maoni gani katika ili? Kumbuka kusambaza makala kwa marafiki nao wasipitwe na makala babkubwa kutoka TeknoKona!

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply