eWater: Mfumo wa kupata maji safi muda wowote kwa njia ya kidigitali

1
Sambaza

Maji ni moja ya kitu muhimu sana kwa binadamu, mimea na hata wanyama. Ni wazi kwamba wasichana/wanawake wamekuwa wakitumia muda mrefu kutafuta maji umbali mrefu kwa ajili ya matumizi ya kila siku. Matumizi ya teknolojia ya eWater imeonekana kuwa mkombozi.

Katika moja ya vitu vilivyoongelewa na kuvutia watu wengi waliohudhuria kongamano la wadau wa TEHAMA lililofanyika Okt. 26-27 2017 ilikuwa ni upatikanaji wa maji safi kwa njia rahisi, salama na inayolinda maji kutopotea kwa karibu asilimia zote ni teknolojia ya eWater.

Bomba la maji safi lililounganishwa na mfumo wa eWater.

eWater ni nini?

eWater ni mfumo wa upatikanaji wa maji safi kwa njia ya kuweka funguo iliyo katika mfumo wa duara mahali fulani na kisha kutumia funguo iliyo katika umbo la duara kwa kuweka kwenye mfumo wa eWater ulipowekwa na kisha maji kuanza kutoka. Ukitoa tu ile funguo na maji yana acha kutoka.

Watoto wakifurahia kupata huduma ya eWater baada ya kuweka ufunguo wa duara kwenye sehehmu inayostahili na maji kuanza kutoka. Ufunguo huo unaweza kutumika saa yote, muda wowote; kila unapotoa ufunguo mfumo unatoa kile kiasi cha maji kilichotumika.

Jinsi mfumo wa eWater unavyofanya kazi.

Mfumo wa eWater unafanya kazi kwa mteja kuweza kunua fuunguo kutoka kwa wakala wa eWater ambaye yeye (wakala) ana nunua vocha kupitia kwenye app ya eWater kulingana na kiasi ambacho mteja amelipia (kima cha chini ni Tsh. 292) na kisha kupewa ufunguo (upo katika umbo la duara) utakaomuwezesha mteja kuweza kupata maji safi mara tu atakapofika bomba la karibu la eWater na kuweka funguo wake sehemu husika na maji kuanza kutoka kwenye bomba.

eWater: Jinsi mfumo mzima unavyofanya kazi.

Mtu yeyote yule anaweza kuwa wakala tu eWater lakini ni lazima awe na simu janja. Kwa kila funguo anayouza kwa wateja wakala ana asilimia fulani ya mapato yanapokuja kugawanywa. eWaterApp haihitaji uwe na kifurushi cha intaneti kwenye simu; inafanya kazi bila intaneti.

Mafanikio yaliyotokana na kutumia eWater.

Mfumo huu mpaka sasa umeweza kupata mafanikio mengi tu ukiachana na kuokoa muda wa karibu saa sita ambao wakina mama waliokuwa wakitumia kwenda kutafuta maji mafanikio mengine ni kama ifuatavyo:-

  • Kuweza kuokoa lita zaidi ya mil. 24 ambazo zilikuwa zinapotea. Hii inatokana na kwamba ukiondoa tu ule ufunguo maji yanakatika.
  • Uwazi wa mapato yanayopatikana kutokana na kutumia mfumo wa eWater ambapo taarifa hizo zinaweza kutumiwa na serikali, mamlaka za maji kuweza kukusanya mapato yao.
  • Upotevu wa maji umepungua kwa asilimia 99.
  • Mabomba kufanyiwa matengenezo ya mara kwa mara ndani ya saa 6 mara tu mafundi wanapopata taarifa kupitia kwenye mfumo wa kidijiti wa eWater.

Mfumo huu unatumika nchini Tanzania (Manyara, Arusha) na nchini Gambia. Mpaka sasa kuna mabomba 200 yanayotumia mfumo wa eWater nchini Tanzania na Gambia. Matarajio ni kufikia watu wengi zaidi mijini na vijini. Unaweza kubofya eWATER kuweza kujua zaidi kuhusu eWater.

Vyanzo: AIPC na eWaterPay

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Kampuni yashtakiwa kutokana na Headphones zinazofanya ujasusi kwa watumiaji wake
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com