Tovuti maarufu ya ExtraTorrent yaacha kupatikana

0
Sambaza

ExtraTorrent ni tovuti iliyojipatia umaarufu mkubwa zaidi kwa jamii ya wanaodownload mafaili mbalimbali kama vile filamu, muziki na magemu mtandaoni hasa hasa pale tovuti nyingine maarufu ya mfumo wa torrent ya KickAssTorrent ilipoacha kutoa huduma pia.

Mtandao huo nguli unaoruhusu watu kudownload bila malipo kazi mbalimbali za kisanii umezima tovuti zake zote (proxy) zilizokuwa zinafanya kazi. Ingawa hawajatoa sababu kuu ila kwa kiasi kikubwa inaonekana itakuwa ni hofu ya kukamatwa hasa hasa baada ya kukua kwa kasi sana katika kipindi cha mwaka mmoja – miwili iliyopita.

extratorrent

Ujumbe wa kwaheri uliokuwa umetolewa katika tovuti ya ExtraTorrent

Umaarufu wake ukamaanisha makampuni mbalimbali yenye hakimiliki ya kazi mbalimbali za sanaa kama vile muziki na filamu wakaongeza kasi ya kuchukua hatua za kisheria na uchunguzi juu ya wanaomiliki mtandao huo.

SOMA PIA:  FAHAMU: Maana Ya 'Fast Charging' Kwa Baadhi Ya Simu Janja!

Je huu ndio mwisho wa familia ya tovuti za Torrents?

extratorrent

Mashabiki wengi wa tovuti hii wamepata majonzi makubwa sana baada ya uamuzi huu

Hapana, miaka na miaka hali imekuwa ikijitokeza. Ila mara zote tovuti moja ikizima nyingine zaidi zinazidi kuinuka na kufanikiwa. Pia kuna mara nyingi mitandao hii inainuliwa tena na mashabiki wake au timu ya watu wengine wachache.

Mfano tovuti nyingine maarufu ya The Pirate Bay tayari ishazimika na hata waanzilishi wake wengine kukamatwa na ata kufungwa lakini mara zote mtandao huo umerudi tena, tena kwa kasi na ubora ule ule chini ya uongozi mwingine wa kisiri.  Tovuti nyingine nje ya ThePirateBay zinazotegemewa kukua zaidi kwa sasa baada ya majanga ya ExtraTorrent ni tovuti za RARBG na YTS/YIFI.ag.

SOMA PIA:  BlackBerry yapata faida: Mapato ya biashara zake yazidi kukua

Je wewe una mtazamo gani juu ya mitandao ya Torrents?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com