Mitandao ya Facebook na Instagram inazindua programu mpya itakayodhibiti muda unaotumiwa na wateja wao katika mitandao hiyo.
Programu hiyo itapatikana katika ukurasa wa ‘settings’ katika mitandao yote miwili baada ya kubofya ‘Your Activity’ katika Instagram ama ‘Your Time’ katika Facebook.
Hatua hii inakuja kufuatia malalamiko kwamba utumiaji wa muda mrefu unaweza kuathiri vibaya afya ya akili. Aidha, watumiaji sasa wataweza kuona kiwango cha muda waliotumia katika mitandao hiyo miwili na kujikumbusha muda waliofikia ili kufunga ujumbe wanaopata kwa muda fulani.
Hata hivyo, watumiaji wengi wa mitandao hiyo wamekuwa na maoni tofauti na ujio wa programu hiyo ambapo wengine wanasema itasaidia kuwazindua kupunguza matumizi ya kukaa kwa muda mrefu mtandaoni.