Facebook Wamerusha Droni Inayosambaza Intaneti

0
Sambaza

Baada ya mshikemshike na vikwazo kwa mpango wao wa FreeBasics huko nchini India, Mark Zuckerberg hajakata tamaa. Kupitia mpango wao wa internet.org, Mark Zuckerberg anaendelea na na matumaini yake ya kuunganisha maeneo yasiyofikiwa na intaneti duniani kwenye intaneti, kwa kutumia droni.

Facebook droni inayosambaza intaneti

Droni inayosambaza intaneti – Picha ya ubunifu wa droni hiyo kama ilivyopostiwa na Zack

Zuckerberg aliandika kwenye ukurasa wake hivi karibuni akisema, “Ninafurahia maendeleo na Aquila, project yetu ya sola inayolenga kutoa huduma ya intaneti katika sehemu zinazopata shida ya intaneti kufika.

SOMA PIA:  iPhone 6s Yaleta Wateja Wengi Kwa Apple Kuliko iPhone 7! #Ripoti

“Tumechukua hatua nzuri za uhandisi na kwa miezi mingi sasa, tumeweza kuirusha kila wiki ndege yetu ya majaribio” Aliandika Zuckerberg kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Hii habari ni nzuri kwa nchi zinazoendelea kwani ni maendeleo yanayoweza kuleta huduma ya intaneti kwenye maeneo magumu kufikia. Hata hivyo, mipango kama hii huwa na dhana mbadala ya kufaidisha kampuni husika na kama tulivoona huko nchini India, amabako wanaharakati wengi waliipinga FreeBasics ya internet.org, huenda Facebook wakapata vikwazo tena kwani droni hapa barani Afrika siyo kitu cha kawaida na sheria zake bado ni changa.

SOMA PIA:  Teknolojia ya Mabasi Yanayoruhusu Magari mengine kupita chini, Sasa kwenye Skendo ya Utapeli

Zuckerberg ameweka picha pia za kuonesha jinsi projekti hiyo inavyoendelea

//

As part of our Internet.org effort to connect the world, we’ve designed unmanned aircraft that can beam internet access…

Posted by Mark Zuckerberg on Thursday, March 26, 2015

Chanzo: TechRepublic, TheGuardian

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com