Facebook Inaangalia Uwezekano Wa Ku'Share Stories Za Instagram Moja Kwa Moja FB! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Facebook Inaangalia Uwezekano Wa Ku’Share Stories Za Instagram Moja Kwa Moja FB!

0
Sambaza

Facebook nao walianzisha Stories kule, lakini cha kushangaza ni kwamba kipengele hicho hakijajipatia umaarufu mkubwa hivyo watu wengi hawakitumii.

http://cieng.com/our-work/sulfur-recovery-unit/

http://alissaalfonso.com/pinta-mi-cuna-completed-baby-cot/ Hapa Facebook inafanyia kipengele hiki majaribio, kipengele hiki kitawezesha mtumiaji wa Instagram kuweza ku’share Stories zake moja kwa moja katika mtandao wa Facebook. Hii dhahiri ni njia moja wapo ya kurudisha kipengele cha FB stories kwa kulazimisha.

go here

Vyanzo mbali mbali vya habari havijapendezwa na taarifa hii na wengi wametoa mawazo yao juu ya hili,  la muhimu kujua ni kwamba Facebook ni mtandao mkubwa sana na una mambo mengi hivyo ni vigumu kwa mtu kuwaza kuwa kuna stories za kuangalia

INAYOHUSIANA  Facebook yalegeza masharti kuhusu matangazo ya sarafu za kidijitali

Kwa mfano Stories zimekua maarufu Instagram na Snapchat kwa sababu mitandao hiyo haina mambo mengi (picha na video) ndio maana inakuwa ni rahisi kuweza kuona Stories

Facebook kuna mambo mengi sana, kuna habari, magroup, page, status, kungalia video n.k ambapo mambo yote haya yanaweza yakafanyika na kumfanya mtu kutofikiria Stories kabisaaaa!

Kwa kuwa hili lipo katika majaribio ngoja tusubiri majibu maana hakuna uhakika kama huduma hii itaanzishwa rasmi au la.

Ningependa kusikia kutoka kwako, hivi umeshawahi kutumia Facebook Stories, niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Kumbuka Kutembelea TeknoKona Kila Siku Kwani Diama Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.