Facebook inafanyia majaribio kipengele kipya kutenganisha machapisho ya kawaida na yale ya kibiashara

1
Sambaza

Unapohitaji watu wengine wajue kitu fulani unaweza ukaweka picha, vido au hata ujumbe wa maandishi kuelezea kitu fulani ambacho kinaweza kuhusu biashara/mambo tu mengine ya kawaida.

Facebook imeona mbali zaidi na kuamua kufanya majaribio ambayo yataleta tofauti kidogo kwa kile ambacho unataka kuchapisha kwenye Facebook na wengine kuona, yaani kama chapisho linahusu biashara basi lichapishwe kwenye ‘News Feed’ ya masuala ya biashara tu na kama ni chapisho la kawaida tu basi liwe kwenye upande wake pia.

SOMA PIA:  Kuusoma ujumbe uliofutwa na aliyeutuma kwenye WhatsApp inawezekana!

Je, jaribio hili lina maana gani kwa wanaomiliki kurasa mbalimbali kwenye Facebook?

Ingawa ni majaribio tu na si rasmi na hivyo kuweza kukubaliwa au kukataliwa kulingana na mrejesho  kutoka kwa watumiaji wa mtandao huo wenye watumiaji wengi zaidi duniani, kitendo cha kuwepo sehemu mbili tofauti kwa ajili ya kuchapisha inaweza ikasababisha wamiliki wa kurasa kuweza kulipia machapisho yao ili yaweze kuonekana kwa marafiki/ndugu kwenye Facebook.

Lakni pia hatua hii inaweza kupanua wigo wa biashara kwa wamiliki wa kurasa kwenye Facebook kwa mantiki ya kwamba machapisho yao yatakuwa yanawafikia watu wengi zaidi.

Sehemu ya kuandika chapisho kwenye Facebook imekuwa ni sehemu kuu ya kushirikisha marafiki kwenye mtandao huu kwa njia ya picha/video na hata maneno.

Jaribio la kuweka vipengele viwili kwa ajili ya machapisho ya kawaida yanapatikana katika baadhi ya nchi tu ambazo ni Bolivia, Cambodia, Guatemala, Serbia, Slovakia na Sri Lanka pia hupenda majaribio hayo yakaendelea kwa miezi kadhaa. Facebook imeweka wazi kuwa haina mpango wa kufanya majaribio hayo kuweza kupatikana duniani kote.

Pia, Facebook haina mpango wa kuwalazimisha wamiliki wa kurasa mbalimbali kulipia kile wanachokichapisha kwenye kurasa hizo.

Je, unadhani kama Facebook wakiamua kuruhusu vipengele viwili vya kuweka machapisho kwenye mtandao wake wa kijamii itakuwa ni uamuzi sahihi au la? Tungependa kujua maoni yako.

Vyazo: Engadeget, Reuters, Telegraph

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com