Facebook Inajaribu Utumiaji Wa Kamera Kama Ya Snapchat!

0
Sambaza

Kama ilivyo katika App ya Snapchat, ukiifungua tuu unaweza ukaanza kuchukua video au kupiga picha (hata katika mfumo wa selfie). Kutokana na mfumo huu wa kamera, Facebook nao wako mbioni kuuleta kwa watumiaji wao.

Kumbuka mfumo huu una mambo mengi ukiachana na kupiga picha/video, baada ya kupiga picha au kuchukua video unaweza ukaongezea mbwembwe katika kazi zako hizo.

Facebook

Muokano Wa Kamera Hiyo Ya Facebook

Kingine ni kwamba baada ya Instagram (ambayo inamilikiwa na Facebook) kuanzisha mfumo wa ‘stories’ ambao inasemekana waliuiga kutoka Snapchat, sasa Facebook na yenyewe imeona iige mfumo wa kamera kama ule wa Snapchat.

SOMA PIA:  VW yajipanga kuhamia katika utengenezaji wa magari yanayotumia umeme

Lakini kwa mtazamo wangu hii ni nzuri pia. Kumbuka kuna mazingira mengine ambayo unaweza kuwa ikawa ni vigumu kwako kuandika status. Fikiria kama huwezi kuandika ‘status’ hiyo si unaweza tuu ukarekodi/ukajirekodi kavideo Fulani hivi ukielezea hali iliyopo?

Facebook

Mfananisho Wa Baadhi Ya Mbwembwe Ambazo Huwa Zinapatikana Katika Kamera Ya Snapchat

Kwa sasa huduma hii inajaribiwa huko nchini Brazil na Canada, pia inakuja na mbwembwe mbwembwe (Filters) nyingi zikihusisha mashindano ya Olympics. Mambo yakijipa na sisi wa huku tutaanza kuifurahia huduma hii pia.

SOMA PIA:  Mwanamke kulipa faini kutokana na kuchati wakati akiwa sinema

Hii inaonekana kwamba moja kati ya malengo makubwa kwa Facebook ni kwamba sasa inataka kujikita sana katika Video, angalia Snapchat ilivyojipatia umaarufu mkubwa kupitia video. Hata Instagram na Facebook baada ya kuanzisha mfumo mzima wa kuweza kutuma video wamejipatia faida nyingi sana.

Angalia Video Hii Uweze Kujionea Kwa Undani Mambo Ambayo Yanaweza Fanyika Kwa Kutumia Kamera Hii

Niandikie hapo chini sehemu ya comment je unaisubiria kwa hamu huduma hii ikufikie katika App yako ya Facebook? Ningependa kusikia kutoka kwako.

SOMA PIA:  Fanya Simu Yako Ya Android Au iOS Itaje Jina La Mpigaji, Ukipigiwa!

Kumbuka Kutembelea TeknoKona kila siku ili kujihakikishia kupata habari na maujanja mbalimbali yanayohusu teknolojia. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com