Facebook inapoteza vijana Marekani, Snapchat inazidi kuwapata

0
Sambaza

Kampuni ya utafiti inayoheshimika nchini Marekani, eMarketer, imesema Facebook inapoteza vijana Marekani wakati app ya Snapchat inazidi kuvutia vijana wengi zaidi.

Kampuni ya eMarketer mwanzoni mwa mwaka jana ilitabili ya kwamba mtandao wa Facebook utapoteza asilimia 3.4 ya watumiaji wa umri wa kati ya miaka 12 hadi 17 kufikia mwisho wa mwaka 2017, data zinaonesha mtandao huo umepoteza watumiaji wengi zaidi ya utabiri huo wa eMarketer.

Facebook inapoteza vijana Marekani, Snapchat inazidi kuwapata

Facebook inapoteza vijana Marekani, Snapchat inazidi kuwapata

Kwa mwaka 2017 mtandao wa Facebook umepoteza asilimia 9.9 ya watumiaji wake wenye umri wa kati ya miaka 12 hadi 17 nchini Marekani, yaani takribani watumiaji milioni 1.4.

SOMA PIA:  WhatsApp: Desemba 31 2017 ndio mwisho kwa simu janja hizi kufanya kazi!

Kwa mwaka 2017 idadi nzima ya watumiaji wa mtandao huo wenye umri wa miaka 12 hadi 17 nchini Marekani ilikuwa ni milioni 12.1.

Mtandao wa Snapchat unazidi kuwa ndio rafiki zaidi kwa vijana nchini humo.

Kwa Marekani mwaka 2018…

  • Snapchat itaongeza watumiaji milioni 1.9 
  • Instagram itaongeza watumiaji milioni 1.6 

Kwa mwaka 2017 Facebook ilipoteza watumiaji milioni 2.8 kwa kundi la chini ya miaka 25 nchini Marekani, shirika la eMarketer limesema kwa mwaka huu watapoteza tena watumiaji milioni 2.1 katika kundi hilo.

SOMA PIA:  Instagram Yafikisha Watumiaji Milioni 800 Kwa Mwezi!

Je wewe unaitumia app ya Snapchat na pia ni mtumiaji wa Facebook? Unamtazamo gani juu ya mitandao hii mitatu ya kijamii? Upi unautumia zaidi?

Chanzo: eMarketer

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com