Facebook kujiweka pembeni na vitu vyenye maudhui ya kutia shaka - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Facebook kujiweka pembeni na vitu vyenye maudhui ya kutia shaka

1
Sambaza

Mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook nambari moja kwa umaarufu na kuwa na watumiji wengi sana kila leo imekuwa ikijaribu kujidhatiti katika huduma yao wanayoitoa kila siku.

purchase lisinopril 40 mg

get link Matukio ya kigaidi ambayo yamekuwa yakitokea kila mara kwa kiasi fulani Facebook imekuwa ikilaumiwa kwa kushindwa kuzuia machapisho ya aina fulani ambayo yalikuwa kama kichochezi kufanikisha jambo fulani.

Mtandao wa kijamii wa Facebook umetoa tamko kwamba unataka kujitenga na mazingira ya uhasama kwa watu wanaoweka maudhui tata au watu wenye viashiria/matendo ya kigaidi.

Kauli hii kutoka Facebook imekuja baada ya matukio ya kigaidi ambayo yaliikumba Uingereza zaidi ya mara moja! na waziri mkuu wa Uingereza, Bi. Theresa May kuzitaka kampuni zinazojihusisha na masuala ya teknolojia kuchukua juhudi za makusudi kukabiliana na maudhui yenye mrengo wa kigaidi.

Mambo mbalimbali yamekuwa yakipata msukumo mkubwa kwenye mitandao ya kijamii na kusababisha maandamano, harakati mbalimbali, n.k.

Ni wazi kwamba makampuni makubwa ya kimtandao zisipokuwa makini zitakuwa zinatoa nafasi kwa vikundi vya wanamgambo wenye itikadi kali kuzaliana. Facebook imetamka kwamba kuanzia sasa itakuwa ikiondoa mara moja, maudhui yenye viashiria vya ugaidi.

http://animalsinthehaus.com/wp-content/plugins/akismet/class.akismet-admin.php Soma pia: Matatani kwa sababu ya kubofya “Like” kwenye Facebook

Mtandao wa Twitter wao wamejinasibu kwamba kazi hiyo yakuondoa ama kufutilia mbali maudhui tatanishi na kamba mwaka wa jana pekee ulifanikiwa kuondoa maudhui ya aina hiyo kutoka katika akaunti elfu nne.

Chanzo: BBC

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  NMB, Halotel kutoa huduma za TEHAMA bure mashuleni
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|