Facebook wametangaza kuanza kutumia HTML5 kucheza video zake katika mtandao kwa vivinjari vyote, hii inamaana kwamba sasa hautahitaji kuwa na plugin maalumu ili kucheza video katika mtandao huo maarufu.
Sababu kubwa kwa mtandao huu kufanya hivyo ni pamoja na kupitwa na wakati kwa plugin maarufu kama flash play.
Kipindi cha nyuma ulikua ukicheza video Facebook basi ilikua inachezeshwa kwa msaada wa kifaa kinaitwa plug in, plug in inatengenezwa na kampuni nyingine (zipo nyingi tofauti tofauti) na sio Facebook. Baada ya kuhudumu kwa muda mrefu plug in zimekuwa na mapungufu mengi hasa ya kiusalama na mitandao kama Facebook imelazimika kuhama aina hiyo ya kuchezesha video ili kuboresha huduma zake.
Facebook wanafikia hatua hii ili kuwavutia watumiaji wake wa mtandaoni kwa kuwapa huduma bora zaidi, katika kutimiza hilo wanataka kuhakikisha kuwa wao ndio chaguo la kwanza kwa watumiaji linapokuja swala la kuangalia na kusambaza video. Mitandao maarufu mingine kama YouTube pia wamekwisha anza kutumia huduma hii ya kucheza video kwa kutumia HTML5.
HTML ni sheria zinazotawala utengenezaji wa kurasa za mitandao, kwa lugha nyepesi hizi ni sheria ambazo lazima zifuatwe na yeyote yule anayetaka kuweka kitu katika mtandao. Mpaka sasa kuna matoleo matano ya sheria hizi na kabla ya hili toleo la tano sheria hizi zilikua hazifafanui juu ya kucheza video hivyo kama unataka ukurasa wako kucheza video ulihitaji kutumia plug in.
No Comment! Be the first one.