Inawezekana tangu ufungue akaunti ya Facebook hujawahi kufikiria kubadilisha au hata kufanya jitihada na hatimae kuweza kubadilisha nywila na kuweka nyingine iliyo imara na madhubuti kwa usalama wa taarifa zako na mambo mengine kwenye Facebook.
Si vizuri kabisa utumie nenosiri hilohilo kwa muda mrefu sana kutokana na sababu za kiusalama na ili kuepuka udukuzi ambao kwa asilimia kubwa unaweza kuepukwa iwapo ukiwa na tabia ya kubadilisha nenosiri mara kwa mara.
Hatua za kufuta ili kubadilisha nywila kwenye Facebook.
- Ingia kwenye mpangilio (settings) kwenye Facebook. Katika masuala mbalimbali kama vile kubadilisha jina, nenosiri, n.k kwenye mpangilio ndio hatua ya kwanza kabisa na itakayokuwezesha kuweza kubadilisha/kurekebisha kulingana na vipengele vilivyopo.
- Bofya kwenye kipengele cha Security and Login. Hii ndio hatua ambayo itafanikisha lile lengo lako la kutaka kubadilisha nenosiri ambalo pengine hujawahi kubadilisha tangu uwe na akaunti ya Facecook au una tabia ya kubadilisha nywila ya kwenye Facebook kila baada ya muda fulani.
Ukiwa ndani ya kipengele cha Security & Login moja kwa moja kwenye ‘Change password‘ na hapo utaweka nenosiri la sasa kisha chini yake utaweka nenosiri jipya na kurudia nenosiri lile katika kipengele kinachofuta.
2 Comments
Comments are closed.