Facebook kufundishwa kama kipengele katika somo la Kiingereza nchini India - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Facebook kufundishwa kama kipengele katika somo la Kiingereza nchini India

0
Sambaza

Facebook ambayo ina watumiaji bil. 1.8 inazidi kuchukuliwa kinamna ya tofauti na kuonekana kuwa kuna umuhimu wa kujumishwa kwenye mitaala katika elimu ya juu huko nchini India.

Facebook ambayo haiwezi kuwa na raha kama hutoweza kusoma kitu fulani kilichochapishwa na mtu kuhusu jambo fulani kwa ajili ya wengine kuweza kujua, kutazama na hata kusema chochote kuhusiana na kile kilichochapishwa.

Uandishi unatakiwa uwe wa kiustadi ili kiweze kuwagusa wengi na hata kupelekea kupendwa na wengi (kama tunavyofanya TeknoKona 😀 ) hivyo kuwa na msukumo wa kile kilichochapishwa kusambazwa kwa wengine na ni wazi kuwa mitandao ya kijamii inaweza kumzolea umaarufu mkubwa mwandishi chipukizi au msanii na kumuwezesha kufikia watu wengi au hata kupata mikataba ya kuchapisha kazi zake kutokana na kile anachokiandika.

http://vancouvermontessori.com/author/vmschools/page/8/ Soma pia: Kamera/mic kwenye laptop ya mwanzilishi wa Facebook ilivyodukuliwa

INAYOHUSIANA  Punguza kupokea maombi ya urafiki Facebook

Chuo kikuu cha Delhi India kinataka kujumuisha kuandika ujumbe wa Facebook kuwa sehemu ya mtalaa wake wa somo la Kiingereza na mambo hayo yamejumuishwa kwenye mswada wa mtalaa wa Kiingereza ambao unatathminiwa na maprofesa wa DU.

Katika tasnia ya kujifunza uandishi mkufunzi mmoja kutoka katika chuo kikuu cha Delhi http://krinkleklean.ca/blogcleaning-tips/ kwamba ujumbe kwenye Facebook utatumiwa kama sehemu ya kozi ya kuimarisha ujuzi – ambayo ni sehemu ya somo inayotumiwa kuwapa wanafunzi maarifa na ujuzi wa kuwawezesha kufaa maeneo ya kazi.

watoto facebook

Katika mtaala huo wanafunzi watakuwa pia wakifundishwa jinsi ya kuandika blogu au barua kuu ya kujitambulisha wakati wa kuwasilisha maombi ya kazi.

http://mnybaalas.org/condolences-on-the-passing-of-christian-vernon/ SOma pia: Udukuzi katika kurasa za Facebook

INAYOHUSIANA  Uganda: Sheria ya kodi ya mitandao ya kijamii kupitiwa upya

DU si chuo kikuu cha kwanza kuanza kutumia Facebook masomoni. Nchini Uingereza, Chuo Kikuu cha Salford huwa na shahada ya uzamivu katika mitandao ya kijamii, ambayo imekuwepo tangu 2009.

Vyanzo: BBC, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.