Facebook Kuifanya Messenger Kuwa Zaidi Ya Messenger! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Facebook Kuifanya Messenger Kuwa Zaidi Ya Messenger!

0
Sambaza

intaneti-apps-tanzania-simu

Sasa tunakaribia kuelewa kwanini Facebook waliifanya App yao ya kuchati, Messenger, kujitegemea na kuwalazimisha watu kuipakua (download) katika simu zao ili waweze kuandika na kujibu meseji zao za Facebook.

Facebook wana mpango wa kuifanya Messenger iwe App inayojitegemea kabisa. Messenger itavuka zaidi mipaka, haitakua kwa ajili ya kuchati tuu. Facebook wametangaza rasmi ya kuwa wanamipango ya kuwezesha watu kuweza kutumiana pesa na kufanya malipo kwa kutumia app hiyo.

Sio hivyo tuu lakini pia Facebook wanatangaza njia ambazo watengenezaji (developers) wataweza kutengeneza app zingine katika mfumo wa huduma na ata michezo(games) zinazoweza kutumiwa ndani ya app hiyo. Kama unatumia Viber basi unafahamu ya kwamba unaweza kucheza gemu kule. Facebook inadhani kuiwezesha Messenger kuwa na matumizi mengi zaidi ya muhimu kutaiwezesha kushindana na App zingine kama ile ya China WeChat na Viber ambazo zina mambo mengi sana ndani yake ukiachana na kutuma na kupokea meseji tuu. WeChat inajihusisha na vitu  kwama malipo ya ‘Peer to peer’, yaani kutumiana.

INAYOHUSIANA  WhatsApp: Wamiliki/Viongozi wa kundi kuamua nani atume ujumbe

Facebook, lengo lao la kwanza kabisa ni kuwatengenezea mazingira mazuri watengenezaji (developers) ambao ndio wenye uwezo mkubwa sana katika kuleta mambo mapya ya kuvutia watu kutumia zaidi app hiyo ya Messenger. Kama hii kitu ikienda poa basi Facebook inabidi wafikirie vitu vipya ambavyo wataviweka kwenye App hiyo (Messenger).

Mpaka sasa haipo wazi kabisa kuwa ni kivipi facebook wana ‘plan’ kufanya yote hayo na ni vipengele gani ambavyo watawaachia watengenezaji (developers) ili kuweza kufanyia kazi. Mtu unaweza tuu kuangalia hata huduma zinazotolewa na WeChat na kujua Facebook wana kazi nzito ya kufanya.

Facebook inatakiwa wawe makini sana wasirudie yale makosa yao ya mwazo.  Kipindi cha nyuma watumiaji wengi wa Facebook walikua wakicheza magemu mengi sana na kupata mialiko ya kucheza magemu hayo, hii haikuwa shwari. Hivyo wengi wanategemea Facebook watajitaidi kutoweka mambo ambayo yatakuwa usumbufu kwa watumiaji wengi.

INAYOHUSIANA  VIdeo za makundi kwenye Instagram sasa ni rasmi

Facebook ni kama mitandao mingine ya kijamii tuu sio wa kwanza kuwafungulia mlango watengenezaji huru (developers) na hata watangazaji kama vile Snapchat walivyofanya, waliweka kipengele cha ‘Discover’ ambacho kilikua na hayo mambo.

Wazo lako ni muhimu, ningependa kusikia kutoka kwako pia tafadhali ungana nasi kupitia kurasa zetu za Facebook ,Twitter, Na Instagram

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Leave A Reply