Facebook Kuja Na "Find WiFi" Kama Kipengele Kipya! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Facebook Kuja Na “Find WiFi” Kama Kipengele Kipya!

0
Sambaza

Facebook kama kawaida yake haijawahi watenga watumiaji wake. Kila siku inajisogeza karibu nao kwa kuwaletea huduma iliyo bora zaidi.

buy augmentin 875 mg

go to site Huduma ya ‘Find WiFi” ni huduma ambayo inategemewa kupatikana duniani kote bure kabisa. Huduma hii itamsaidia mtumiaji wa Facebook kugundua ni sehemu gani (karibu na alipo) kuna huduma ya WiFI inayopatikana bure.

Mwaka jana huduma hii ilikua inapatikana katika simu za iOs kwa baadhi ya nchi ambazo zilikua zimechaguliwa. Huduma hii ilikua ikipatikana kama sehemu ya majaribio. Baada ya mambo kwenda sawa basi Facebook imeona haina budi kuisambaza huduma hii dunia nzima

Pata picha unaweza ukawa hauna bundle la kutosha ila kwa kutumia mtandao wa Facebook unaweza ukatonywa wapi kuna WiFi ya bure karibu. Unaweza ukajongea eneo hilo na ukafanya yako bila tatizo!

Kingine kizuri ni kwamba ukiwa ndio unatafuta WiFI ya bure, itakuja listi ambayo imejaa majina ya sehemu ambazo kuna WiFI ya bure na vitu vinavyofanyika humo (mfano, mgahawa n.k)

Orodha Ya WiFi Zilizopo Karibu Na Huduma Zinazopatikana

Facebook kwa sasa inawatumiaji Bilioni mbili kwa kila mwezi. Jambo hili ni zuri na kuweka huduma ya ‘Find WiFi’ ndio kabisa wanazidisha kupata watumiaji ambao watakuwa wanatumia facebook kama njia ya kutambua biashara zilizopo karibu

INAYOHUSIANA  Punguza kupokea maombi ya urafiki Facebook

Kwa mfano mtu atakua hana haja tena ya kuingia Google ili kujua sehemu ya karibu ambayo anaweza kwenda kunywa kahawa. Akifungua facebook tuu sehemu ya ‘Find WiFi” anaweza kaona sehemu nyingi tuu ambazo anaweza kwenda kwa mfano anaweza akaona migahawa mingi yenye WiFi.

Find WiFi Ikiwa Katika Eneo La Ramani

Unapotafuta WiFi za bure, itatokea ramani ya ambayo itakua inatoa vialama juu ya sehemu ambazo kuna WiFi ya bure. Ukichagua eneo moja wapo pia unaweza ukapata maelekezo juu ya namna ya kufika katika eneo hilo husika.

Ningependa kusikia kutoka kwako, wewe hili unalionaje kutoka Facebook? Niandikie hapo chini sehemu ya comment.

Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.