Facebook kuja na Mfumo wa Magemu - kama vile Steam - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Facebook kuja na Mfumo wa Magemu – kama vile Steam

0
Sambaza

Kampuni ya Facebook kwa kushirikiana na kampuni nyingine Unity Technologies zimeungana katika kutengeneza mfumo wa mauzo na manunuzi ya magemu. Facebook kuja na mfumo wa magemu kama vile ule wa Steam (bofya hapa kufahamu kuhusu Steam).

http://clearhelp.org/tag/lvdm/ mfumo wa magemu wa facebook

http://wmswirt.com/lansing-building-products/ Inaonekana kwa kiasi kikubwa Facebook na Unity wanajitahidi kuona kama wataweza kunufaika na ukuaji mkubwa wa biashara ya magemu ya simu na yale ya kwenye mtandao wa Facebook. Taarifa zinaonesha Facebook na Unity wanatengeneza programu ya PC iliyo kama programu maarufu duniani ya mauzo ya magemu ya kompyuta – Steam.

purchase femara online Inamaanisha ukishapakua programu hiyo utaweza kununua na kupakua magemu kwenye kompyuta yako ata kama magemu hayo yametengenezwa kwa ajili ya kuchezeka kwenye mtandao wa Facebook tuu. Kampuni ya Unity Technologies ni bingwa zaidi katika teknolojia zinazotumika katika utengenezaji magemu ya mtandaoni na ya kwenye simu.

INAYOHUSIANA  Facebook yapoteza wateja kutokana na GDPR

mfumo wa magemu facebook

Na ni kupitia teknolojia za kampuni ya Unity inasemekana ata magemu ya iOS na Android yataweza kupatikana na kupakuliwa kwenye kompyuta kupitia programu hiyo. Pia kutakuwa na maboresho makubwa yatafanyika katika mtandao wa Facebook.com ili kuboresha mfumo wa magemu katika mtandao huo.

Je huwa unacheza magemu katika mtandao wa Facebook?

 

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.