Facebook kujenga ‘Data centre’ New Mexico badala ya Utah

0
Sambaza

Kila mfanyabiashara anaangalia faida kutokana na biashara anayofanya/anayotaka kufanya. Kutokana na kodi kubwa huko Utah, Facebook kujenga data centre New Mexico baada ya tathimini ya kina kufanyika.

Baada ya hali ya usalama kuimarika huko New Mexico Facebook wamevutiwa na kuamua kujenga Data Centre mpya. Facebook ilikutana na viongozi wa New Mexico na kukubaliana kuhusu ujenzi huo na ujenzi huo utaanza mwezi Oktoba. Data centre hiyo itakuwa ni ya saba kujengwa na kumilikiwa na Facebook.

Data centre itakayojengwa New Mexico kuanzia Mwezi Oktoba.

Data centre itakayojengwa New Mexico kuanzia Mwezi Oktoba.

Data Centre (kituo cha kuhifadhia kumbukumbu) hiyo inatarajiwa kujengwa katika kijiji cha Los Lunas kilichopo pembezoni mwa New Mexico. Hapo awali kulikuwa na mpango wa kujenga Data Cenre huko Utah lakini kutokana kodi kubwa inayotozwa Utah Facebook wamesmua kuwekeza New Mexico.

Mfano wa kituoo cha kumbukumbu (Data centre) kitakachojengwa New Mexico.

Servers maalum kwa utunzaji wa kumbukumbu kwenye Data centre.

New Mexico imeamua kusamehe kodi ya mali (property tax) katika uwekezaji huo kwa miaka 30 na badala yake wanakuwa wakilipwa $50,000|zaidi ya Tsh. bil. 110  (kwa kuanzia) kila mwaka kwa muda wa miaka 30.

Uwekezaji wa Data Centre unafanya biashara ya cloud computing (uwifadhi wa taarifa sehemu ya ‘kufikirika‘) kuzidi kuimarika ingawa uwekezaji huo hutoa ajira chache kwa wenyeji wa eneo husika kutokana na kazi nyingi zinahitaji ujuzi wa kitaalamu na sio nguvu za mikono.

SOMA PIA:  Google Jamboard: Ubao janja wenye ukubwa wa inchi 55

Katika kuvutia uwekezaji ni muhimu sana kubuni njia ambazo zitawavutia wawekezaji na njia mojawapo ni kusamehe kodi. Kutokana New Mexico imesamehe kodi hiyo imefanikiwa kuwavutia Facebook na kuwekeza New Mexico.

Vyanzo: ABC News, the guardian

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com