Facebook kuruhusu watumiaji wake kufuta kumbukumbu ya walichotafuta - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Facebook kuruhusu watumiaji wake kufuta kumbukumbu ya walichotafuta

0
Sambaza

Mtandao maarufu wa Kijamii wa Facebook umetangaza kuongeza faragha kwa watumiaji wake kwa kuweka sehemu ya kufuta historia ya walichokitafuta (search) katika mtandao huo wa kijamii.

follow url

Mtandao huo umefikia uamuzi huo baada ya hivi karibuni kukumbwa na kashfa ya kutolinda faragha za watumiaje wake huku zaidi ya watu 50 millioni wakidaiwa kudukuliwa taarifa zao katika kipindi cha uchaguzi wa Marekani.

Inaelezwa katika sakata hilo mamilioni ya taarifa za watumiaji zilichukuliwa bila ridhaa na kampuni ya Cambridge Analytical kwa matumizi ya wanasiasa. http://dollfacemake-up.com/home/feed Mkurugenzi Mtendaji na mwanzilishi mwenza wa Facebook, Bw. Mark Zuckerberg aliwahakikisha watumiaji wa mtandao huo kwamba suala kama hilo halitajitokeza tena kwa kuweka ulinzi zaidi.

kufuta kumbukumbu

Bw. Mark, Zuckerberg ambae amekuwa akipambana kadri awezavyo kuweza kurudisha heshima ya Facebook ambayo imetoweka baada ya kampuni hiyo kukumbwa na kashfa kubwa zaidi miezi michache iliyopita.

Kupitia mkutano wa mwaka wa kampuni ya Facebook Mark, Zuckerberg alisema kwamba kilichotokea kwa Cambridge Analytical ni uvunjifu wa uaminifu wa hali ya juu, wakichukua data za watu na kuziuza hivyo watahakikisha suala hilo halitokei tena kwa kuweka vizuizi kwa data ambapo can you buy lasix over the counter mtu atakua anaombwa kwa ridhaa yake, na kuondoa programu zote mbaya zilizopo kwenye mtandao huo wa kijamii.

Uimarishwaji huo wa ulinzi kwa Facebook sasa utamruhusu mtumiaji wake kuweza kufuta historia ya kile alichokitafuta kupitia mtandao huo.

kufuta kumbukumbu

Sehemu ambayo unaweza kuopndoa programu tumishi, michezo, n.k ambayo uliiunganisha na akaunti yako ya Facebook.

Kutokea kwa kashfa ya matumizi ya taarifa za watumiaji wake kumeifanya Facebook kuendelea kufanya marekebisho kadhaa ili kurudisha imani ya watumiaji wake wengi walionza kuingia mashaka ya kudukuliwa taarifa zao.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Facebook na Instagram zinapambana kudhibiti uraibu
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.