Facebook Light, App kutoka Facebook Isiyotumia Data Nyingi

0
Sambaza

Facebook wanakuja na app rasmi wanayoiita Facebook Light yaani ‘Facebook nyepesi’ kwa ajili ya mitandao ya 2G na EDGE, au kwa kifupi zaidi tunaweza sema ni kwa ajili ya intaneti isiyo na kasi sana. Kwa kiasi kikubwa app hii inategemewa iongoze utumiaji wa Facebook zaidi kwa watu ambao app ya sasa hivi huwa inakuwa nzito katika kufungua vitu n.k kutokana na utumiaji wake mkubwa wa intaneti (data).Facebook-Lite-640x376

Je kuna tofauti gani kubwa?

Moja ya tofauti kubwa ni ata ukubwa wa faili la kushusha kwa ajili ya kuweka app hiyo kwenye simu yako.  App hii inachukua nafasi ya takribani MB 1 baada ya kuwekwa kwenye simu ukilinganisha na app rasmi ambayo kutegemea na simu yako inaweza kuchukua hadi zaidi ya MB 100 kwenye simu zingine. Facebook Light inaukubwa wa takribani kb 252 wa kushusha (download), wakati app rasmi huwa inaukubwa wa takribani MB 25.

SOMA PIA:  Ifahamu Tecno Camon CX (Toleo La Manchester City), Sifa Na Uwezo! #Uchambuzi

Muonekane wake pia ni muonekano mwepesi usio na mambo mengi sana ya kiubunifu kama ile app tuliyoizoea. Kwa kiasi kikubwa wamejitaidi kuweka katika hali ya kawaida karibia kufanana na mtu ukienda mtandao wa Facebook wa simu, yaani m.facebook.com ila tofauti kuu kuwa kupitia Facebook Light utapata taarifa za haraka (notifications) moja kwa moja kwenye simu yako kama vile app ya kawaida ya Facebook.

Kingine kikubwa ni utaweza kuchati kama kawaida kwenye Facebook Light bila kuitaji app nyingine, Facebook Messenger, kama simu nyingine nyingi.

SOMA PIA:  Simu ya Rais Donald Trump ina App moja tu!

Pia hautaweza kucheza/kutazama video ndani ya app hiyo, ukibofya taarifa (post) ya video itakupeleka kwenye kivinjari (browser) yako, uitazame huko.

Kwa sasa hivi app hii inapatikana kwenye Google Play kwa baadhi ya simu tuu, na pia si kwa nchi zote. Inapatikana kwa nchi za Zimbabwe, Bangladesh, Nepal, Nigeria, South Africa, Sudan, Sri Lanka, na Vietnam. Ila kwa kuwa tunakujali tumefanikiwa kupata faili la APK kwa ajili ya simu za Android. Kumbuka kuweza kuweka (‘install’) app hii kwenye simu yako lazima uruhusu ‘setting’ ya ‘Unknown Sources’ kwenye simu yako ya Android.

SOMA PIA:  App ya DU Recorder: App ya kurekodi screen/display yako

Bofya hapa kuweza kushusha na kuweka app hii kwenye simu yako ya Android -> Facebook Light

Facebook wamedai kutokana na utafiti walioufanya na unaoweza kugunduliwa na watumiaji pia, ni kwamba app hii inatumia data kidogo kwa zaidi ya asilimia 50 kulinganisha na app ya kawaida ya Facebook.

Je utashusha app hii na kuijaribu? Tuambie kama umefanikiwa na umeipenda au la. Kumbuka unaweza ungana nasi pia kupitiaTwitter, Facebook Na Instagram!

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com