Muanzilishi wa Facebook, abadili mtazamo wake juu ya dini

Muanzilishi wa Facebook, Mark Zuckerberg abadili mtazamo wake juu ya dini

0
Sambaza

Kwa muda mrefu bwana Mark Zuckerberg amekuwa na msimamo wa kuwa katika kundi lisiloamini katika dini yoyote, yaani ‘atheist’ ila kwa sasa inaonekana anabadili mtazamo.

go to link Mark Zuckerberg abadili mtazamo wake juu ya dini..

Bwana Mark Zuckerberg

follow site Bwana Mark Zuckerberg

http://bcascouting.org/frequently-asked-questions-2/ Suala la yeye kuona umuhimu wa dini kwa sasa umeonekana katika post aliyoiweka Facebook akiwatakia watu heri ya Krismasi. Katika post hiyo mtu mmoja alimpiga swali na kumuuliza ‘Wewe si hauamini dini?’ alijibu, ‘Hapana, nililelewa katika dini ya kiyahudi na nilipitia kipindi ambacho nilikuwa na udadisi wa kila jambo, ila kwa sasa naamini dini ni muhimu sana’

Hakuingia kwa undani sana ila kwa kiasi kikubwa inaonekana muda si mrefu atakuwa wazi zaidi juu ya hilo.

INAYOHUSIANA  Punguza kupokea maombi ya urafiki Facebook

Mke wake anahasili ya nchini China na ni mfuasi wa dini ya kibudha – Buddhism, na katika safari yake ya nchini China mwaka 2015 Zuckerberg alionekana katika tempo moja ya maombi kwa ajili ya wafuasi wa budha. Na alisema ameagizwa na mke wake amsaidie kusema maombi kadhaa eneo hilo.

Kundi lisilo amini katika dini limezidi kukua na hasa hasa kwa nchi zilizojuu kiuchumi. Katika makundi ya kiimani kundi la wasioamini masuala ya dini lilikuwa ni la tatu kwa wingi kufikia mwaka 2012, nyuma ya ukristo (watu zaidi ya bilioni 2.2) na waislam(watu zaidi ya bilioni 1.6).

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.