Facebook marufuku kuchukua data za watumiaji wa WhatsApp Ujerumani

Facebook marufuku kuchukua data za watumiaji wa WhatsApp Ujerumani

1
Sambaza

Kampuni ya Facebook imejikuta kwenye kikaango cha sheria huko Ulaya baada ya kupigwa marufuku kuchukua data za watumiaji wa WhatsApp Ujerumani.

Baada ya WhatsApp kubadilisha mikataba ya utumiaji kwa watumiaji wa app hiyo maarufu duniani kote tayari watu pamoja na mashirika mbalimbali yanayolinda haki za usalama data za watumiaji wa huduma za kimitandao walilalamika.

http://bobbiekinkead.com/tamingoftiger/ facebook whatsapp ujerumani

order colchicine canada Kamishna wa Ulinzi na Usalama wa Data wa jiji la Hamburg huko nchini Ujerumani ametoa hukumu leo akiitaka Facebook kuacha mara moja kuchukua data kutoka kwa watumiaji wa WhatsApp nchini Ujerumani.

buy modafinil online overnight Pamoja na hilo Facebook wametakiwa pia kufuta data zote za watumiaji wa WhatsApp ujerumani ambazo tayari wameshachukua.

Mabadiliko yaliyoletwa kwenye appb ya WhatsApp kwa kiasi kikubwa yamechangiwa na huduma hiyo kumilikiwa na Facebook.  Facebook walilipa bilioni 19 za dola za kimarekani kuinunua WhatsApp mwaka 2014, na njia pekee ya kurudisha pesa hizo ni kuangalia ni kwa namna gani wataweza kunufaika kibiashara kutoka kwenye data zinazohusu mamilioni ya watumiaji duniani kote.

Je ni nini kitafuata?

Kuna uwezekano mkubwa wa mataifa mengine ya Ulaya kuchukua hatua kama hii. Hili likitokea basi Facebook wanaweza jikuta wakifanya mabadiliko kwenye huduma hiyo ili iwe ni chaguo la mtu kabisa kama anataka data zinazohusu utumiaji wake wa WhatsApp zipelekwe pia Facebook au la. 

Kikubwa ni suala hilo kuwa kiuwazi kabisa na si la kilazima.

Vipi wewe unalionaje suala la Facebook kutaka kujinufaisha kibiashara kwa kutumia data/taarifa zinazohusu utumiaji wako wa WhatsApp, aina yako ya simu na taarifa zingine nyeti?

Chanzo; Telegraph.co.uk na mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Udukuzi wa taarifa za wateja unatesa mabenki
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |