Facebook Messenger: Sasa utaweza kupiga simu za makundi (Group Calls)

0
Sambaza

Facebook wametangaza kuanza kuwezesha uwezo wa kupiga simu kwa watu wengi kwa wakati mmoja (Groups calls) kwa watumiaji wa Android na iOS ndani ya app ya Facebook Messenger.

Habari hiyo iliyotangazwa na mkuu wa Facebook Messenger bwana David Marcus kupitia mtandao wa Facebook utawawezesha watumiaji wa Facebook Messenger kupiga simu na kuwezesha mazungumzo ya watu wengi kwa wakati mmoja.

source facebook messenger  kupiga simu za makundi

Kwa njia rahisi ya kubofya eneo la alama ya kupiga simu ndani ya kundi la watu unaochat nao mtumiaji ataweza kuwapigia simu wote waliokwenye kundi hilo kwa wakati mmoja….na hivyo kuweza kufanya mazungumzo kwa wote.

buy synthroid 150 mcg Uwezo huo wa kupiga simu umewekwa wa hadi kupiga simu kwa watu 50 kwa wakati mmoja, ili kuwezesha uwezo huu mpya katika app ya Facebook Messenger unatakiwa usasishe (update) app hiyo na kisha ndani masaa kadhaa utaweza ona uwezo huo ukiingia kwenye chat ya group.

INAYOHUSIANA  WhatsApp kuja na muonekano wa giza

Facebook wanazidi kuleta mapya ndani ya app ya Facebook Messenger kwani watu wengi bado wanaona ulazima wa kuwa na app hiyo haupo kwa sana. Na pia inaonekana Facebook wanalengo la kutaka kuwa app namba moja kwa ajili ya mawasiliano ya kila siku.

Je una mtazamo gani na teknolojia hii? Umeijaribu? Tungependa kusikia kutoka kwako.

Chanzo: FirstPost na mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.