Facebook Messenger Mbioni Kuja Na Mazungumzo Ya Siri! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Facebook Messenger Mbioni Kuja Na Mazungumzo Ya Siri!

0
Sambaza

Kampuni la Facebook kwa ujumla linafanya maboresho mengi sana katika huduma zake mbali mbali, mfano Instagram wamekuja na sekunde 60 katika video na Messenger mbioni kuja na ‘Secret Conversation’.

generic Fincar without prescription canada

go site Hii inamaanisha kuwa ‘ buy femara canada Secret Conversation’ (Mazungumzo ya siri) yatakuwa yakifanyika katika Messenger baina ya mtu na mtu. Sawa tuna App nyingi sana siku hizi za kutuma na kupokea meseji na kila moja ina faida na hasara zake. Licha ya facebook kuwa moja wapo inaonekana dhahiri kuwa wapinzani wake wanaipa tumbo joto.

Facebook Messenger

Facebook Messenger

Facebook licha ya kuwa inajiboresha yenyewe kama yenyewe lakini bado kwa kiasi kikubwa inaangalia wapinzani wake wanafanya nini. Ukifikiria mpango mzima wa ‘Secret Conversations’ wazo moja linaweza likakujia kwamba kipengele hicho kinaweza kikawa kinafanana na kipengele cha SnapChat cha huduma za meseji za kupotea ndani ya muda mchache mara baada tuu ya kusomwa au muda wake kupita (expire).

INAYOHUSIANA  Fahamu Mambo Mapya Yanayokuja Kutoka WhatsApp

Pengine labda inaweza ikawa sio meseji za kupotea kama za SnapChat lakini kitu cha kutegemea ni kwamba mazungumzo ambayo yatakuwa yakifanyika ndani ya kipengele cha ‘Secret Conversation’ yanaweza yakawa ya usiri zaidi katika macho ya watu wengine

Mpaka sasa hakuna taarifa kamili kuwa hiyo ‘Secret Conversation’ itakuwa vipi au itakuwa na vitu gani ndani. Cha msingi ni kusubiria taarifa maalumu kutoka kwa Facebook Messenger wenyewe.

Muonekano Wa Ndani Ya Facebook Messenger

Muonekano Wa Ndani Ya Facebook Messenger

Hapa kuna mambo mawili kwani inawezekana ikawa maongezi hayo ya siri yakawa yamefichwa kiasi cha kwamba hata serikali ikashindwa kuyajua au ikawa tuu ni kuyaficha kwa ajili ya macho wa watu wa kawaida tuu – ndio moja kati ya hilo linawezekana au yote kwa ujumla — katika kutumia mtandao wa facebook.
Hii inaweza ikamaanisha kuwa watumiaji wa Messenger wanaweza wakaamua kuficha baadhi ya mazungumzo labda kwa kutumia nenosiri na mazungumzo mengine wakayaacha wazi wazi tuu.

INAYOHUSIANA  Ifanye akaunti yako ya YouTube ikuingizie pesa

Tusubiria ripoti ya uhakika zaidi kutoka kwao Messenger, lakini kizuri ni kwamba tupo mbioni kupata huduma bora zaidi kutoka kwao kwani wanajali usiri wetu.

Ningependa kusikia kutoka kwako juu ya jambo hili, niandikie sehemu ya comment hapo chini. Pia tembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku kwa habari moto moto za kiteknolojia. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.