Facebook Waja na Messenger ya Mtandaoni

0

Tayari tulishaandika kuhusu maamuzi ya Facebook ya kuboresha zaidi huduma yao ya kuchat ya Messenger – Soma – Facebook Kuifanya Messenger Kuwa Zaidi Ya Messenger!. Katika kuzidi kuonesha uboreshwaji wa huduma hiyo kampuni hiyo imetumia anuani yao ya www.messenger.com kwa ajili ya huduma hiyo.

Kwa sasa mtu ataweza kuingia kwenye mtandao huu wa www.messenger.com akiwa kwenye kompyuta na kuweza kuchati bila kwenda kwenye mtandao wa Facebook dot com.

messenger-screen-shot

Muonekano wa Messenger katika kivinjari

Kwenye mtandao huo bado utaweza kutumia vitu kama vile stika, utumaji wa picha na kikubwa zaidi eneo zima la kuchati litakuwa linajaa kwenye eneo lote la kivinjari (browser). Pia utaweza kupiga simu ya sauti na ya video.

Wengi wanasema cha kutegemea muda si mrefu ni kwamba kampuni hiyo inaweza amua kutengeneza programu ya kompyuta kabisa na hivyo kushindana moja kwa moja na Skype. Maboresho unayotakiwa kuyategemea hivi karibuni ni pamoja na uwezo wa kuchati kwenye Messenger na makampuni, yaani ‘Brands’ na ata kufanya manunuzi ya kimtandaoni kutumia Messenger.

Soma pia – Facebook Kuifanya Messenger Kuwa Zaidi Ya Messenger!

Endelea kutembelea TeknoKona.com

–> Masaa machache baada ya huduma hiyo kuanza ilipotea tena kwenye mtandao huo na inasemekana ni kutokana na tatizo la kiufundi na maboresho yanafanyika

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com