Katika kile kinachoonekana kama maboresho makubwa katika matumizi ya mtandao wa kijamii wa Facebook, kipengele cha kuweza kuhariri picha katika tovuti kimeongezwa.
Uwezo huu umekuja ikiwa ni wakati ambao tayari katika apps nyingi za mitandao ya kijamii zina uwezo kufanya uhariri wa picha mnato na video.
Uhariri huu umeongezwa kwa wale ambao wanatumia Facebook kwenye tarakilishi (apps) au kwenye mtandao moja kwa moja. Ingawa sini hii bado haijapatikana kwa watu wote, inaonekana kuwa katika siku chache zijazo kila mmoja ataweza kuhariri picha zake, kubadilisha kiwango cha mwanga na kuchuja rangi.
Uongezwaji wa sini hii unakuja wakati ambao kuna muendelezo wa mapambano ya uboreshaji wa huduma za mitandao ya kijamii, ikifuatia karibu mitandao yote ya kijamii ikiwekeza katika kuwezesha mtumiaji kwenda mubashara (live)
Jinsi ya kujaribu:
Endelea kuwa nasi kuwa wa kwanza kupata kila taarifa mpya ya kiteknolojia inapotokea. Pia usisahau kuweka maoni yako hapo chini kuhusiana na habari hii na habari nyingine katika mtandao huu.