Facebook wanunua App ya Filter maarufu – MSQRD

0
Sambaza

Mtandao maarufu wa Facebook umefanikiwa kujimilikisha App ya filter za video ya MSQRD iliyokuwa inamilikiwa na kampuni ndogo ya Masquerade  ambayo inajishughulisha nakutengeneza app kwaa jili ya filter ya picha na video.

Kitendo ambacho kinatafsiriwa na wengi kuwa ni hatua ya kuongeza mapambano dhidi ya mtandao maarufu wa Snapchat ambao nao umekuwa ukishika kasi kwa kupendwa na watu.

App ya MSQRD pia ni maarufu sana kwa uwezo wake wa kuweza kuchomoka sura mbalimbali katika picha nyingine – face swap.

SOMA PIA:  Nova Launcher yapakuliwa mara milioni 50 mpaka sasa

Hivi karibuni Snapchat walinunua  Looksery ambayo iliwapa mafanikio makubwa  Facebook wameona jinsi watu walivyoipokea filter hizi katika app ya Snapchat na pengine hii ikawa ndio sababu ya wao kununua app hii ya MSQRD.

airtel tanzania bando

app ya filter MSQRD

Ingawa gharama rasmi za dili hili hazija tangazwa lakini Facebook wamekubali katika blogu yao kwamba wamenunua App hiyo. Inahisiwa kwamba Facebook wataanza kuizitumia filter za app hii katika app yao ya Messenger.

Kwa Facebook dili hili lina maana kwamba sasa wataweza kushindana na Snapchat ambao umekuwa mtandao tishio kwa mitandao mikubwa na mikongwe ya kijamii, sasa wataweza kuwapa watumiaji wao vitu ambavyo awali viliwafanya wakimbilie Snapchat – Je watafanikiwa? Ni vigumu kujua kwa sasa.filter

SOMA PIA:  Jinsi ya kusambaza kitu chenye ujazo mkubwa kwenye WhatsApp #Maujanja

Ukiachia mbali pesa ambazo wamiliki wake wamezipata baada ya kukubali kumilikiwa na Facebook Masquarade wao hii ni nafasi yao kutumia miundombinu ya Facebook (fedha ikiwamo) kwa ajiri ya kujiimarisha na kutengeneza bidhaa bora zaidi.

Na kwa sisi watumiaji wa Facebook tukae mkao wa kula maana baada ya muda sio mrefu tutaanza kuona aina ya filter ambazo tunaziona Snapchat zikiwa zinatumiwa zaidi Facebook au ata kwenye Instagram. Hii ni kwa sababu Facebook wamesema wataiacha MSQRD iendelee kivyake ila watatumia baadhi ya vitu katika apps zao.

SOMA PIA:  Watu wawili tu ndio hutaweza kuwa'bloku' facebook!

Usisahau kusambaza makala kwa marafiki, na kuweka maoni yako katika eneo la kucomment..

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com