WATCH: Facebook yaanza kutoa huduma mpya ya video

0
Sambaza

Facebook yaanza kutoa huduma mpya ya video. Mtandao huo namba moja wa kijamii duniani unatarajia kuanza kutoa huduma ya video itakayokuwa ikiitwa ”Watch” ama tazama.

Teknolojia hiyo imebuniwa ili kushindana na televisheni za kawaida pamoja na mitandao ya Youtube, Netflix na Twitter (kupitia huduma zao za LIVE).

Facebook yaanza kutoa huduma mpya ya video: Kupitia tab ya Video WATCH ndani ya mtandao huo inalenga kuvutia watazamaji wa tamthilia na michezo, hii ikiwa ni pamoja na vipindi vya mubashara – yaani LIVE.

Facebook yaanza kutoa huduma mpya ya video

Facebook yaanza kutoa huduma mpya ya video

Facebook inasema kwamba imewekeza mamilioni ya dola katika kuifanya huduma hiyo kupendwa zaidi.

SOMA PIA:  Google yakiri kuwafuatilia watumiaji wa simu janja za Android

Facebook tayari ina vipindi kadha vikiwemo vya michezo, vya familia na vya televisheni ya National Geographic.

Watch itaanza kupatikana kwa watumiaji wa nchini Marekani kabla ya huduma hiyo kuanza kusambaa kwa watumiaji wengine duniani kote.

Chanzo: BBC na mitandao mbalimbali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com