Moja kati ya vitu ambavyo vinazidi kutanuka ni matumizi ya sarafu za kidijitali na kuona makampuni mbalimbali, mabenki, mashirika ya ndege, n.k kukubali aina hiyo ya malipo.
Ukiwauliza idadi kubwa ya watu hasa kwetu Afrika na Tanzania kwa ujumla wake ni wachache sana kati ya wengi watakwambia kuwa ukiwekeza kwenye sarafu ya kidijitali inalipa lakini asimlimia kubwa ya watu watakwambia “Ni uwongo na wala usithubutu kuwekeza huko, utatapeliwa“.
Facebook ni moja ya makampuni ambayo yalikatza kabisa matangazo yanayohusu sarafu za mtandaoni baada ya kuona matangazo hayo yanakosa ukweli na kupotosha. Katazo hilo lilianza tangu mwezi Januari 2018.
Katika tangazo walilotoa Facebook hivi karibuni wameamua kuondoa katazo la matangazo yanayohusu fedha/sarafu za kidijitali lakini matangazo ambayo yataruhusiwa ni kwa wale tu ambao wameidhinishwa na wahusika (Facebook) mara baada ya maombi yao kupitiwa na kukubaliwa.
Vitu vinavyohitajika wakati wa kupeleka maombi ya tangazo linalohusu sarafu ya kidijitali.
Ingawa masharti yamelegezwa kiasi chake lakini bado Facebook inataka kujiridhisha kuwa kweli mwombaji ana vigezo walivyoviweka; ni lazima kuambanisha leseni ya biashara, uthibitisho iwapo wameshawahi kufanya mauzo kupitia soko huria (DES kwa Tanzania) pamoja na nyaraka nyingine yoyote inayofaa kuongezea ili tangazo lako lipitishwe. Lakini vigezo hivyo vinaweza kubadilika kulingana na mrejesho kutoka kwa watu. BOFYA HAPA ili kuweza kujaza fomu.
Ili kufanikiwa katika kitu chochote ni lazima usiwe na hofu ya kuthubutu na vivyo hivyo kuwekeza kwenye sarafu za kidijitali inakubidi uwe na nia ya kuthubutu ili uweze kuona faida zake.
Tanzania ni moja ya nchi ambazo inaliangalia suala zima la fedha hizi zisizoshikika kwa jicho la pili.
Vyanzo: Engadget, Recode
One Comment
Comments are closed.