fbpx

Facebook yapoteza wateja kutokana na GDPR

0
Sambaza

Facebook ambayo ilikuwa ikipata wateja wengi/watu wanaojiunga na mtandao huo wa kijamii safari hii mambo yamekuwa ni tofauti na sababu kuu ikiwa ni kutokana na GDPR iliyoanza kufanya kazi hivi karibuni.

next

Makampuni mengi hivi sasa yanatoa takwimu ya kilichopata katika robo ya pili ya mwaka na kwa upande wa Facebook mambo si shwari tofauti na ilivyokuwa imezoeleka kwa kampuni hiyo kubaini kuongezeka kwa watumiaji wa mtandao huo wa kijamii ambao una watu wengi sana wanaoutumia.

Facebook imepoteza wateja hai/wa kila mwezi karibu miloni moja na kufikia milioni 376 kutoka bara la Ulaya huku sababu ikiwa ni GDPR (General Data Protection Regulation).

GDPR ni nini?

GDPR ni sheria inayolinda taarifa za watu ikijumuisha faragha kwa wanachama wa umoja wa Ulaya pamoja na maeneo yote ya kiuchumi yanayozunguka umoja huo. Sheria hiyo ilipitishwa na bunge la umoja wa Ulaya na kuanza kutumika Mei, 25 2018.

kutokana na GDPR

Kuwepo kwa sheria hii ni mwiba kwa Facebook na baada ya anguko hilo hivi sasa ina watumiaji wa kila siku wapatao 2.2bn duniani kote.

Pia inaaminika sakata la Facebook na Cambridge Analytica limechagia idadi kubwa ya watu kuacha kutumia mtandao huo wa kijamii ingawa wachambuzi wengi wanasema GDPR inawabana makampuni kama njia ya kulinda taarifa za watu.

Vyanzo: Engadget, AdAge

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Kivinjari cha Samsung ni maarufu! Sasa kimepakuliwa zaidi ya mara bilioni 1
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.