Facebook yashindwa kesi kuzuia kushtakiwa - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Facebook yashindwa kesi kuzuia kushtakiwa

0
Sambaza

Msichana mwenye umri wa miaka 14 amedhamiria kuichukulia hatua za kisheria kampuni fulani ili kuweza kulipwa kutokana na Facebook kuruhusu picha ya utupu ya msichana huyo kuwekwa katika ukurasa wa “Shame page” katika mitandao ya kijamii.

Jaji wa mahakama ya juu mjini Belfast (huko Uingereza) imemruhusu kuweza kuishtaki kampuni hiyo. Msichana huyo ameenda mbali zaidi na source url anataka pia kumchukulia hatua za kisheria mvulana aliweka picha ya utupu ya msichana huyo. Kesi ya namna hiyo itakuwa ni ya kwanza kuwahi kusikilizwa nchini Uingereza.

Iwapo binti huyo akishinda kesi huwenda akalipwa mamilioni ya dola kutoka Facebook.

go site Iwapo binti huyo akishinda kesi huwenda akalipwa mamilioni ya dola kutoka Facebook.

Msichana huyo anatafuta haki yake kutokana na Facebook  kutumia vibaya taarifa binafsi, kudharau na kuruhusu picha hiyo kuwekwa kwenye mtandao wa kijamii (Facebook) na pia kukiuka masharti ya sheria za kutunza taarifa za watu kwa nchi husika.

Facebook imekuwa ikiandamwa na mikono ya sheria mara kadhaa, inaweza ikalipa pesa nyngi ikipatikana na hatia.

see Facebook imekuwa ikiandamwa na mikono ya sheria mara kadhaa, inaweza ikalipa pesa nyngi ikipatikana na hatia.

Picha hizo zinasemekana kuwekwa mtandaoni kati ya  Nov 2014 and Jan 2016. Hata hivyo wakili wa Facebook aliiomba mahakama ifute madai ya msichana huyo kwani Facebook wamekuwa wakijitahidi kuzuia kuakikwa kwa picha zisizofaa na Facebook imekuwa ikondoa picha mbaya mtandaoni mara tu zinapobainika.

INAYOHUSIANA  Facebook ina mbinu ya kuwa karibu na mkufunzi

Katika miaka ya karibuni mitandao ya kijamii kwa ujumla wake wamekuwa wakali katika ufuatiliaji wa picha, mambo tunayoandika (status) yasiyofaa katika jamii. Ni muhimu kuzingatia sheria na maadili kuepuka matatizo.

Vyanzo: The guardian, maltatoday

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.