Facebook yawezesha kutuma picha zenye ubora wa 4K kwenye Messenger - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Facebook yawezesha kutuma picha zenye ubora wa 4K kwenye Messenger

0
Sambaza

Facebook imekuwa kiungo muhimu sana katika kurahisisha mawasiliano kwa kwenye Facebook bila hata kufungua app kuu ya Facebook na ukafungua tu Facebook Messenger na ukaweza kujibu ujumbe na hata kupiga/kupokea simu kupitia kwenye Facebook Messenger.

http://millbrookyoga.com/2016/02/more-news-from-india/

enter Mbali na kutuma/kupokea ujumbe kwenye Facebook pia mtumiaji anaweza kutuma nyaraka, picha, video na aliyetumiwa akawa na uwezo wa kuona na kufungua kile kilichotumwa lakini kwa kwenye upande wa kutuma/kupokea picha kwenye Facebook Messenger ndio sasa Facebook imeangalia kwa jicho la ziada na kuboresha.

Facebook imebainisha kuwa takribani picha bil. 17 zinasambazwa kila mwezi duniani kote lakini tangu huko nyuma Facebook where can i purchase lasix iliruhusu picha za kiwango cha 2K kuweza kutumwa/kupokelewa. Picha zaubora wa  2K au 4K unategemeana na kifaa (kamera, simu, n.k) iliyopga picha husika.

Mfano wa picha iliyo katika ubora wa 2K.

Katika masasisho ambayo yameanza kupatikana kwenye Facebook Messenger mtumiaji wa Facebook Messenger anaweza kutuma picha iliyo katika ubura wa 4K tofauti na hapo awali ambapo Facebook ilikuwa ikikubali picha za kiwango cha ubora wa 2K.

Upande wa kushoto ni picha ya kiwango cha 2K na upande wa kulia ni picha ya kiwango cha 4K.

Tofauti kati ya picha ya kiwango cha 2K na 4K.

Teknolojia inavyozidi kukua na ndivyo vitu vinazidi kuboreshwa na kuleta kitu kitu/mambo mapya kwenye ulimwengu wa teknolojia. Tunapozungumzia picha ya ubora wa kiwango cha 2K au 4K ina maana ya muunganiko wa vipande vidogo vidogo (pixels) ambapo zikiungana kwa pamoja ndio picha kamili inatokea.

INAYOHUSIANA  Honor 9N yazinduuliwa

Picha ya ubora wa 2K uwiano wake unakuwa ni karibu vipande vidogo vidogo 2,000 huku uwiano wa picha za kiwango cha 4K ukiwa ni 4096 x 4096 pixels. Picha za 4K zina muonekano ang’avu sana kulinganisha na ubora wa picha za 2K. Kujua zaidi kuhusu pixels BOFYA HAPA!

Picha ya kiwango cha 4K (upande wa kulia) ni ya kiwango cha juu sababu inayoifanya kuwa na MB nyingi kuliko ile ya 2K (upande wa kushoto) ukiituma.

 

Sasisho hili limeanza kupatikana Marekani, Kanada, Ufaransa, Australia na Uingereza. Kwa nchi nyingine Facebook inatarajia kuruhusu sasisho hilo katika siku za usoni. Vipi umefurahisha na kile kilichoboreshwa kwenye Facebook Meesenger?

Vyanzo: The Verge, Engadget

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.