Fahamu Emoji 38 Mpya Zinazokuja Kwenye Simu janja Zetu

0
Sambaza

Mfumo wa teknolojia inayotuwezesha kutumia Emoji katika simu zetu upo njiani kupitia na kuthibitisha ongezeka la Emoji nyingine 38 katika teknolojia hiyo. Na Emoji hizo mpya zitakuwa ni tamu kweli kweli.

Shirika linalosimamia mambo ya Emoji, linafahamika kwa jina la Unicode Consortium , ndilo linalosimamia maendelea na marekebisho ya teknolojia ya Unicode 9 ambayo ndio inatumiwa katika simu janja zetu kuwezesha utumiaji wa Emoji. Shirika hilo limepokea Emoji mpya 38 ambazo zinategemewa kuanza kusambazwa kwa watengenezaji programu endeshaji za simu (Android, iOS, n.k) na kuwezesha Emoji hizo mpya kuanza kutumika kufikia kati kati ya mwaka 2016.

SOMA PIA:  Marekani: Kirusi cha WannaCry kimetoka Korea Kaskazini

Je kuna nini kipya?

Bwana Harusi!4 emoji mpya Bwana Harusi

Kulikuwa tayari na Emoji ya bibi harusi na sasa bwana harusi pia anaongezwa.

Mshikaji anayecheza muziki1 Emoji mpya - kucheza mziki

Tayari kulikuwa na emoji ya binti anayecheza muziki na hakuna ubishi saa nyingine ata sisi wanaume tunataka kutuma emoji ya kucheza tukimaanisha washikaji wajiunge nasi viwanja…ondoa hofu, tutakuwa na emoji yetu pia.

Mke wa Santa/Baba Krismasi2 emoji mpya - mke wa santa

Tayari kulikuwa na Emoji ya Santa mwanaume, na sasa kutakuwa na emoji ya mke wake pia

SOMA PIA:  Drone ya kubebea mzigo wa zaidi ya kilo 200 yaundwa

Mtoto wa Kiume wa Mfalme (Prince)3 emoji mpya - king - mtoto wa mfalme

Tayari kulikuwa na emoji ya binti wa mfalme na sasa kutakuwepo na nyingine spesheli kwa ajili ya wakaka

Mjamzito5 emoji mpya - mjamzito - mimba

Wadada ondoeni shaka, hamtaitaji kuandika maelezo mengi kusema ya kwamba wewe ni mjamzito… kutakuwa na emoji spesheli inayopunguza urefu wa maneno. 🙂

Sura zaidi6 emoji mpya - sura mpya

Je sura zilizopo kwenye emoji za sasa hazitoshi kuelezea kila kitu? Basi ondoa shaka, kuna sura nyingine mpya zitaongezwa.

Alama za Vidole7 emoji mpya mikono

SOMA PIA:  Teknolojia ya FaceID kwenye iPhone X 'yamvuruga' John Cena

Tushukuru bado ile emoji ya kidole cha kati inayoombwa na wengi bado hawajaifikiria kuiweka. Hizi ndizo alama za vidole unazoweza kuzitumia muda si mrefu.

Usafiri

Kuna Emoji zimeongezwa kwa ajili ya kuonesha vyombo vingine vya usafiri

Je ni Emoji gani imekuvutia zaidi katika hizi? Ungependa kuona za aina gani zije?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com