#Fahamu - Fursa katika Ujasiliamali wa Kiteknolojia - TeknoKona Teknolojia Tanzania

#Fahamu – Fursa katika Ujasiliamali wa Kiteknolojia

0
Sambaza

Ujasiariamali unahubiriwa kila kukicha, hasa hapa nyumbani kwetu Afrika ambapo upatikanaji wa kazi unazidi kuwa changamoto.

Moja ya sekta zinazotiliwa mkazo zaidi kwenye mahubiri haya ni ujasiliamari unaohusikia na teknolojia. Hii ni kwa sababu teknolojia inakuwa kwa kasi ya kuridhisha barani Afrika.

Picha Na the-star.co.ke

Picha Na the-star.co.ke

Viashiria vya Ujasiliamari -Teknolojia Kukuwa

Si muda mrefu sana tangu raisi Barack Obama wa Marekani, kufungua mkutano wa dunia wa ujasiliamali ulioikuza zaidi Kenya kuwa kitovu cha teknolojia Afrika, Global Entrepreneurship Summit (GES). Yapo mengi yalizungumziwa kwenye mkutano huo ikiwemo kuskuma wakinadada (wanawake) kwenye nyanja ya ujsiliamari-teknolojia. Kufuatia hilo na hata kabla ya ujio wa Obama, kumekuwa na ongezeko la nguvu ya kisiasa inayokubali kwamba teknolojia ndiyo itakayakomboa waafrika kutokana na ujinga, umasikini, maradhi, njaa na changamoto zingine zinazowakabili Afrika.  Zaidi ya hapo, pia ni vizuri kutambua kwamba kuna jumuia za wanateknolojia zinazozidi kuzuka kila kona ya Afrika. Watu wanakuja pamoja, kushirikishana na kukuza

Kwa nini uingie huku?

Kuna biashara nyingi unazoweza kufanya na kujinufaisha ila biashara inayohusika na teknolojia ni bora. Kwa upande wake, faida kubwa ni kuwa soko hili bado ni changa na kuna fursa pana za kuwekeza na kupata faida kubwa. Teknolojia inavuka mipaka kirahisi na hivyo soko ni pana sana ukiwa na mawazo ya mbali.
Unaweza ukajiuliza sasa hivi ni jinsi gani unaweza kuingia kwenye biashara ya teknolojia wakati hauna ujuzi wowote kwenye kusuka ‘code’ au kutengeneza programu wala kuunganisha vifaa vya kielektroniki. Hapa inafaa ujue kwamba ushirikiano upo na ujuzi ni juu yako. Kuna njia nyingi na utitiri wa taarifa zitakazokupa urahisi wa kufanya mambo.

Ufanye Nini ili Ufanikiwe?

Moja ya njia za kufanikiwa inayoshauriwa ukiwa na wazo la kibunifu na kiteknolojia ni kujiunga na “Incubator hubs.” pamoja na jumuia za wanateknolojia. Kwenye ‘hubs’ utakuta watu wa kukuongoza, kukupa ushirikiano kwenye kukuza biashara na hata kukupatia mtaji.

Hapa Tanzania zipo BUNI Hub na KINU! zilizopo jijini Dar es Salaam. Hizi ‘hus’ zinaongoza kwa sasa ila zipo nyingine kadhaa nchi nzima zinazolenga kutoa nafasi ya kukuza vipaji na biashara za teknolojia. Kenya ipo I-Hub, Nailab na nyingine kadhaa. Afrika kote zipo sehemu kama hizi zinazoshirikiana kimataifa.

Mitaji Ipo

Kuhusu mitaji, yapo mashindano na makampuni kadhaa hapa afrika na kutoka nje. Pia kuna watu wapo tayari kuwekeza kwenye teknolojia kwa sababu wanaamini kwamba biashara inaelekea huko.
Soma zaidi hapa kuona orodha ya makampuni, incubators na mashindano yaliofanya kazi ya kufadhili na kukuza biashara ya teknolojia amabayo unashauriwa kufuatilia mwaka huu.

click Katika dunia ya sasa, biashara ya teknolojia inazidi kuwa rahisi kuanzisha na kumudu. Teknokona inakushauri ufikirie na kuthubutu kuanzisha biashara kwenye uwanja huu. Je, una mawazo zaidi ungependa kuwasilisha? Ungana nasi.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ninafuatilia teknolojia kila siku na ninapenda kutoa ujuzi wangu kuhusu teknolojia. Karibu tuzungumze kuhusu teknolojia hapa teknokona!

Leave A Reply