Fahamu Jinsi Ya Kufuta (Delete) Na Kuzima (Deactivate) Akaunti Ya Instagram!

0
Sambaza

Kwa taarifa zilizotoka mwezi Julai ni kwamba mtandao wa Instagram una zaidi ya watumiaji milioni 500 ambao wanatumia mtandao.

Hiyo ni namba kubwa sana kwani ukilinganisha ni mitandao mingi ya kijamii ambayo inataka kufikia namba hiyo ya watumiaji. Lakini ngoja nisitoe sifa nyingi za mtandao huo wa Instagram kwani nyingi zinafahamika.

Kama umetumia Huduma za Instagram na ukachoka, ukaamua kupumzika kuitumia au ukaamua kujitoa kabisa katika mtandao huo. Usipate tabu kwani leo TeknoKona itakufunza yote.

Kujitoa Kwa Muda – Deactivate.

– Fungua mtandao wa Instagram kwa kutumia kivinjari (browser) usitumie App ya Instagram. Unaweza ukafanya hivyo kwa kutumia simu janja yako au hata kompyuta

SOMA PIA:  Kongamano la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) kufanyika Oktoba 26 na 27, Dar Es Salaam

Log in katika akaunti yako ambayo unataka kuipumzisha kwa muda

– Nenda katika Profile lako na kisha ingia katika Edit profile

– Shuka chini kisha chagua ‘Temporarily Disable Account

Futa Instagram Kwa Muda

Futa Instagram Kwa Muda

– Baada ya hapo stepu itakayofuata itakua ni kujaza sababu ya kwanini umeamua kupumzisha akaunti hiyo.

– Ukimaliza kujaza hapo sasa nenda katika ‘Temporarily Disable Account’ na kisha Bofya OK

Zima Instagram Kwa Muda

Zima Instagram Kwa Muda

Mpaka hapo utakuwa umeipumzisha akaunti yako ya Instagram kwa muda (Kwa lugha nyingine unakuwa bado hujaifuta kabisa japokuwa watu wanaotumia mtandao huo hawataweza kukuona ndani ya mtandao)

SOMA PIA:  Google kufanya masasisho ya kwenye apps zake kuongeza usalama

Siku ukiamua kufufua akaunti yako na kuanza kuitumia tena njia ya kukuwezesha kufanya hivyo ni rahisi sana. Hapa cha kufanya inakubidi ufanye kama unavyo Log in kawaida siku zote. Ukishaingiza jina/barua pepe na neno siri lako, akaunti yako itafunguka.

Kuifuta Akaunti Moja Kwa Moja – Delete

Njia hii ni tofauti kidogo na hiyo ya yapo juu. Hii ni kwa wale watu ambao wanataka kufuta akaunti zao kabisa. Cha muhimu kuzingatia hapa ni kwamba ukishafanya njia hii HUTAWEZA tena kupata akaunti yako (itakuwa imefutika kabisa).

SOMA PIA:  Teknolojia ya Mabasi Yanayoruhusu Magari mengine kupita chini, Sasa kwenye Skendo ya Utapeli

– Kama ilivyokua hapo juu, ingia katika mtandao wa Instagram kwa kutumia kivinjari hasa hasa tumia kompyuta na kisha Log in

– Kisha Fuata Ukurasa Huu ili kufuta akaunti yako

– Baada ya hapo itakubidi uingize sababu kwanini unafuta akaunti hiyo na kisha uingize neno siri

– Baada ya hapo ingia katika ‘Permanently Delete My Account

Futa Kabisa Akaunti Ya Instagram

Futa Kabisa Akaunti Ya Instagram

Mpaka hapo ni mategemeo yangu kuwa umeweza kufanikiwa katika yote haya. Niambie umeshindwa wapi hata hivyo. Niandikie hapo chini sehemu ya comment, ningependa kusikia kutoka kwako.

Tembele TeknoKona kila siku kwa habari na maujanja mbalimbali yanayohusu Teknolojia kwa ujumla. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com