Rununu ni moja ya kitu ambacho kinatuwezesha kufanya mawasiliano kwa haraka na hata kurahisisha shughuli mbalimbali lakini kutokana na ukuaji wa teknolojia kufahamu iwapo simu zako zinafuatiliwa ni jambo muhimu sana.
Katika dunia ya leo watu wanapenda kujua vitu vingi kwenye teknolojia kiasi kwamba mtu anaweza kujikuta anatokea kujihusisha kwa namna moja au nyingine kwenye ulingo huo.
Mbali na hapo kutokana na sababu mbalimbali mtu mwingine anaweza akatumia mbinu fulani fulani kutaka kufahamu mambo yanayoendelea kwenye simu ya mtu mwingine na iwapo utakuwa na mashaka/kutaka kujua iwapo kuna mtu anafuatilia mawasiliano yako ni muhimu kuwa hatua moja mbele zaidi yake.
Jinsi ya kujua kama mtu anafuatilia mazungumzo yako kwenye simu.
i kitu rahisi sana na inakubali kwenye simu janja au hata zile za “Kawaida”. Piga *#61# angalia kama italta majibu “FORWARDED“ basi ujue kuna mtu anafuatilia mazungumzo/ujumbe mfupi wa maneni. Na iwapo itaonyesha neno “NOT FORWARDED” basi uko salama.
Kuondoa au kumzuia mtu asiendelee kutumia namba yako piga ##21# ili kuondoa mazungumzo yako kuchunguliwa kwenye namba yako.