Fahamu Kuhusu Viatu Janja Kutoka Lenevo! #Teknolojia

0
Sambaza

Ilivyotoka saa janja tuliona kama ni kitu cha ajabu mpaka tukaja kizoea (mimi nimeshazoea) lakini uzuri wa teknolojia ni kwamba unachokiona leo ni cha ajabu kesho utakiona ni cha kawaida sana

Lenovo wao wamemua kuleta teknolojia ya kiatu (viatu) janja. Viatu hivi ni spesheli kwa wale wanokimbia huku vikiwa na mbwembwe kibao za kiteknolojia

Viatu Janja Kutoka Lenevo

Viatu Janja Kutoka Lenovo

Baadhi Ya Vitu Ambavyo Kiatu Janja Hicho Kinaweza Fanya

> Kutumika Katika Kuongoza Gemu – Ili kuendena na wakati. Kampuni imeamua kugawa mamlaka katika viatu janja hivyo ya kuweza kuongoza michezo mbalimbali katika simu janja. Kwa msaada wa viatu hivi wachezaji wanaweza wakacheza gemu kwa kwenda kushoto au kulia, kuruka na kuweza kufanya mambo mengine mengi ndani ya gemu husika. Kumbuka pia hata kwa yale magemu ya kucheza (Dancing Games) viatu hivi vinaweza vikawa ndio chaguo sahihi

SOMA PIA:  Zifahamu Kope Janja (F.Lashes)!

> Hifadhi Ya Taarifa Za Afya – Viatu hivi sio tuu kwa ajili ya kutembelea tuu, pia vinasimamia swala zima la Afya ya mtumiaji. Viatu hivi vina skana ya 3D ambayo inapatikana katika soli inatumika katika kuangalia Afya ya mtumiaji. Skana hiyo ina uwezo wa kugundua kiwango (asilimia) cha mafuta cha mwili, kiasi cha jasho linalotiririka wakati wa mazoezi na uzito wa mtu.

> Viatu Hivi Vinawaka Kwa Chini – Viatu hivi vina taa za mfumo wa LED ambazo zinapatikana katika upande wa chini kabisa wa viatu hvi. Hii ni msaada mkubwa sana kwa wale wanaofanya mazoezi (sana sana ya kukimbia) katika nyakati za usiku. Kingine ni kwamba inasemekana taa hizi zinaendana na mdundo wa muziki pale unaposikiliza muziki.

Taa Ya Viatu Janja Hivi Kwa Chini

Taa Ya Viatu Janja Hivi Kwa Chini; Hapa vikichajiwa

Kizuri kuhusiana na kiatu hiki ni kwamba kila mtu anaweza akavaa maana kina muonekano wa kawaida tuu. Yaani sio lazima uwe unafanya mazoezi ndio uweze kuvaa kiatu hiki bali hata kwa matumizi ya kawaida unaweza ukakivaa.

Muonekano Wa Viatu Janja Hivyo Kutoka Lenovo

Muonekano Wa Viatu Janja Hivyo Kutoka Lenovo

Lenovo haikuingia ndani sana kuhusiana na kiatu hiki. Haikusema ni malighafi gani ilitumia, bei bado haikuwa wazi.

SOMA PIA:  Marufuku kuwauzia watoto saa janja za 'kitoto' Ujerumani

Angalia Video Hii Kujionea Zadi Kuhusu Kiatu Janja Hiki

Tuambie maoni yako juu ya swala hili kumbuka kupitia TeknoKona.Com tumeshasoma sana kuhusu saa janja na hivi juzi juzi tuu tumesoma kuhusu mswaki janja na leo kiatu janja, nini unahisi kitafuata katika tasnia ya teknolojia? Niandikie sehemu ya comment hapo chini. Ningependa kusikia kutoka kwako.

Tembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku kwa habari za kijanja zinazohusu teknolojia kwa ujumla.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com